Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Timu ya Taifa ya England jana imeweza kutoka kidedea baada ya kuwafunga wapinzani wao, Scotland, mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Wembley.
Mabao ya England yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 29, Danny Welbeck dakika ya 53 na RickieLambert dakika ya 70, Scotland ilitangulia kupata mabao yake kupitia kwa Morrison dakika ya 11 na Miller 49.
Kikosi cha England kilikuwa Hart, Walker, Cahill, Jagielka/Jones dk84, Baines, Cleverley/Milner dk67, Gerrard/Oxlade-Chamberlain dk62, Wilshere/Lampard dk46, Walcott/Zaha dk75 na Rooney.
Scotland: McGregor, Hutton, Martin, Hanley, Whittaker, Snodgrass/Conway dk66, Morrison/Rhodes dk82, Brown, Forrest/Mulgrew dk67, Maloney/Naismith dk86, Miller/Griffiths dk73.




Kazi kazi tu: Rooney alipiga mzigo wa nguvu dhidi ya Scotland na katika dakika ya 67 alisababisha bao la ushindi

0 comments:
Post a Comment