Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
“Balaa United”, wakati mabingwa soka nchini England, Manchester United wakiwasili leo asubuhi Bangkok na kupokelewa na mashabiki lukuki tayari kwa kuanza ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, mshambuliaji ambaye kwa sasa hajatulia klabuni hapo, Wayne Mark Rooney amelazimika kurejea nchini England na kuachana na ziara hiyo ikiwa ni siku moja tu tangu United wasafiri nje ya nchi.
Klabu imesisitiza kuwa mshambuliaji huyo wa England ambaye muda mwingi amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford majira haya ya usajili ya kiangaza, amepata majeraha ya nyama za paja, hivyo ameruhusiwa kurudi nyumbani,
Taarifa ilisema ” “Kutokana na maumivu ya paja aliyopata katika mazoezi, imeamuliwa kuwa Wayne Rooney lazima arudi nyumbani haraka iwezekanavyo kwa ajili ya matibabu zaidi”.
“Atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja”


Habari za kuondoka kwa Rooney United zimepata nguvu tena, hivyo bado utata unabaki pale pale kama nyota huyo atabaki Old Trafford msimu ujao.
Wakati hayo yakitokea, kocha mpya wa United, David Moyes alishasema kuwa Rooney haondoki na hauzwi, ingawa amepitisha taarifa kuwa mchezaji huyo amethibitisha kuwa amekubali kubakia klabuni.
Jana, Moyes aliwaambia talkSPORT: ‘ Klabu imesema Wayne atabakia klabuni hapa na hauzwi. Nimekutana na Wayne mara mbili, tatu,nne na ndio maana yupo hapa”.


0 comments:
Post a Comment