Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Meneja wa Liverpoo Brendan Rodgers anatarajia kufanya usajili wa nyota wengine mwezi ujao kwa malengo ya kuboresha kiwango cha majogoo hao wa jiji msimu ujao wa ligi kuu, ikiwezekena kutwaa ubingwa au kushika nafasi nne za juu na kucheza ligi ya mabingwa barani Ualaya.
Nyota wanne waliowasili Anfield kwa maana ya kipa kutoka Sunderland Simon Mignolet, beki kutoka Manchester City, Kolo Toure, mshambuliaji kutoka Celta Vigo, Iago Aspas na kiungo kutoka Barcelona B, Luis Alberto – wote kwa ujumla wamekiimarisha kikosi hicho kwa mujibu wa Rodgers.
Lakini kumkosa kiungo wa Shakhtar Donetsk Henrik Mkhitaryan, aliyejiunga na Borussia Dortmund, wekundu hao wa Anifield wanahamishia rada zao kwa wachezaji wengine wanaoweza kuwasainisha ili kuongeza nguvu zaidi.
Kuhusu Luis Suarez, Rodgers amesema sauala hilo liko wazi kuwa klabu yake haina mpango wa kumuuza nyota huyo raia wa Uruguay, licha ya Arsenal kujipanga kutuma ofa nyingine Anfield.

Wewe na yule mnaelewa: Brendan Rodgers yuko makini kununua wachezaji wapya majira haya ya joto ya usajili ya kiangazi ili kuimarisha kikosi cha majogoo wa jiji msimu ujao
Nyota mpya: Mlinda mlango Simon Mignolet, akionesha vitu vyake, na ni miongoni mwa nyota wanne waliosajiliwa majira haya ya kiangazi
Kazi kwelikweli: Kolo Toure, ambaye amejiunga na Liverpool akitokea Manchester City, akijaribu kushusha pumzi wakati wa mazoezi ya klabu hiyo leo
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya Asernal kumkosa Gonzalo Higuain kutka Real Madrid, sasa wamehamishia nguvu zao zote kwa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez na wanajiandaa kutuma ofa ya pauni milioni 30 ambayo ilikataliwa wiki iliyopita.
Lengo la Liverpool ni kuongeza wachezaji wapya: Mipango ya kuisuka upya timu yetu inakwenda vizuri na lengo kubwa ni kununua wachezaji wengi tunaoweza kuwalipa”. Alisema Rodgers
Iago Aspas, aliyesajili majira haya ya kiangazi kutokea Celta Vigo, akiwa mazoezini
0 comments:
Post a Comment