
William Halule (kushoto) na Elirehema Maturo(Kulia) wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakitoa maelezo kwa baadhi ya wageni waliotembelea banda la TTB lilioko katika jingo la wizara ya Maliasili na Utalii katika maonesho ya Kimataifa ya Dar es salaam.
………………………………………………
Idadi
kubwa ya wananchi wanaopata fursa kutembelea banda la Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) lililopo ndani ya jeno la Wizara ya Maliasili na Utalii
wanaoneka kuhamasika zaidi na suala zima la Utalii wa ndani ambalo TTB
inaonekana kulipa msukumo wa pekee kwa lengo la kuhakikisha watanzania
wanahamasika kutembelea vivutio vilivyomo katika nchi yao na kuondokana
na dhana kuwa vipo kwa ajili ya wageni tu kutoka nje ya nchi.
Hali
hiyo imedhihirisha katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere barabara
ya Kilwa jijini Dar es salaam ambapo wananchi wengi wamekuwa wakiulizia
na kupata ufafanuzi zaidi kuhusu umuhimu wa wao kutembelea vivutio vyetu
na suala zima la kukuza utalii wa ndani huku wengi wakionesha
kuhamasika kutembelea vivutio hivyo.
Wananchi
wengi ambao wamekuwa wakitembelea banda la Bodi ya Utalii wamekuwa
wakidadisi zaidi kuhusu gharama za kutembelea vivutio mbalimbali na
umuhimu wa utalii wa ndani katika kuinua uchumi wa nchi. Aidha wamekuwa
wakihoji kuhusu vivutio vya Tanzania vilivyoshinda na kuingizwa katika
orodha ya maajabu Saba ya Asili Barani Afrika ambavyo ni Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti (kwa maana ya nyumbu wahamao) Kreta ya Ngorongoro, na
Mlima Kilimanjrao.
Pamoja
na kushiriki katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii lilioko
katika viwanja hivyo vya maonesho, Bodi ya Utalii Tanzania inashiriki
pia katika banda la PTA sambasamba na Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) na Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA). Banda la PTA mwaka
huu ni mahsusi zaidi kwa makampuni na waoneshaji kutoka nje ya nchi.
Maonesho
hayo yaliyoanza tarehe 28/06/2013 na kushirikisha waoneshaji kutoka
ndani na nje ya nchi yanatarijiwa kuhitimishwa tarehe 8/7/2013.
0 comments:
Post a Comment