Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Wakati
kocha mpya wa mabingwa wa soka nchini England, Manchester United, David
Moyes akianza kazi rasmi jana, taarifa za nyota wake Wayne Roney
kutimka Old Trafford bado zinaendelea kushika kasi, licha ya leo wawili
hao kukutana kujadili hatima ya nyota huyo msimu ujao.
Imeelezwa
kuwa Rooney na Moyes wamekutana kabla ya kuanza ziara ya maandalizi ya
ligi msimu ujao, lakini taarifa zizizotokea leo lakini sio rasmi,
zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa mazungumzo yanakwenda vizuri
huku wakala wa Rooney bwana Paul Stretford na mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward wakishiriki katika majadiliano hayo nyeti.

Anataka
kuondoka? Wayne Rooney, ambaye alifurahia wikiendi iliyopita maeneo ya
Glastonbury, bado anaonekana kuwa na nia ya kuondoka licha ya leo kuwa
katika mazungumzo na David Moyes
…………………………..
Moyes
bado hajakata tamaa ya kumshawishi Rooney kuendelea kuitumikia klabu
hiyo, lakini mbivu na mbichi zitajulikana leo baada ya mazungumzo ya
wawili hao.
Wawakilishi
wa Rooney wameonekana kumshinikiza nyota huyo kutimka United kufuatia
mambo yaliyojitokeza msimu uliopita ambapo mpachika mabao huyo alipoteza
nafasi mbele ya Robin Van Persie, lakini kilichomuumiza kichwa sana ni
kuwekwa benchi na Sir Alex Ferguson katika michezo muhimu hususani ligi
ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Kaota mbaya United: Rooney wikiendi hii alikuwa anakula bata maeneo ya Glastonbury fakiwa na mke wake Coleen.

Rooney
ni miongoni mwa wachezaji wa United watakaoenda mashariki ya mbali
katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini England
ambapo watakuwa wanatetea ubingwa wao
0 comments:
Post a Comment