Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Washika
bunduki wa jijini London nchini England wakiwa chini ya kocha wao
Mfaransa, Aserne Wenger wameinasa saini ya nyota kinda wa kimataifa
kutoka nchini Ufaransa, Yaya Sanogo kwa kumpa mkataba mrefu Emirates.
Kinda
huyo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya umri
wa miaka 20m katika fainali za Kombe la Dunia la vijana chini ya umri
wa miaka 20 huku akiwa amefumania nyavu mara mbili kati ya matatu ya
timu yake nchini Uturuki.
Akicheza
ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa, Sanogo amefunga mabao tisa
katika mechi 13 huku akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.

Mtu mwenye dili kwa sasa: Sanogo amejijengee nafasi nzuri sana katika taifa la Ufaransa

Nyota
wengine wa kutua Emirates? Higuain (kushoto) na Rooney (kulia) pia wapo
katika rada za Wenger ambaye anataka kupata nyota wakali wa kuimarisha
kikosi chake msimu ujao
Gonzalo
Higuain na Wayne Rooney wameripotiwa kuwa katika mipango ya Wenger
msimu ujao, lakini kocha huyo raia wa Ufaransa amevutiwa na kinda
Sanogo.
‘Sanogo
ni mchezaji mzuri sana atakayesaini kwetu, ameonesha kiwango kikubwa
katika klabu yake ya Auxerre na katika kikosi cha timu ya taifa chini ya
umri wa miaka 20″. Alisema Wenger.
0 comments:
Post a Comment