Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
wa zamani wa klabu ya Darajani, Chelsea Ray Wilkins anaamini miaka 10
ya umiliki wa Roman Abramovich umeibadili timu hiyo ya England kuwa
mbaya zaidi.
Jumatatu
ya jana, Abramovich alitimiza miaka 10 akiwa ni mmiliki wa klabu hyo na
katika utawala wake ametwaa mataji matatu ya ligi kuu na makombe ya
mabingwa barani ulaya.
Wilkins, ameliambia gazeti la The Sun: ‘Chelsea kama bidhaa yetu, imeibadili kuwa nzuri lakini kuna makosa”.
‘Kwa
timu yetu ya England, imekuwa mbaya zaidi. Kwa bahati mbaya katika
miaka 10 ya Roman kumekuwepo na ujio wa wachezaji wengi kutoka nje ya
England, hivyo kuwanyima nafasi wazawa kucheza klabuni hapo”.Alisema
Wilkins.
Wilkins
ambaye aliwahi kuichezea Chelsea miaka ya 1970, ana amini kuwa sera ya
bilionea huyo kuchukua wachezaji wengi wa kigeni imeharibu maendeleo ya
soka la England.

Mtumiaji
na mwenye jeuri ya pesa: Matumizi makubwa ya pesa ambayo hufanywa na
Abramovich kusajili wachezaji ghali kutoka nje ya England kumekuwa na
mchango hasi katika maendeleo ya soka la England, amesema Wilkins.

Akiwa kibaruani enzi zake: Wilkins (kulia) alikuwa kocha wa Chelsea chini ya Abramovich kati ya mwaka 2008 na 2010


Wilkins aliongeza: ‘Tumeona timu imekuwa na mafanikio makubwa na kuwa bora zaidi duniani, lakini imeleta hasara kubwa”.
‘Tumeona
jinsi ambavyo kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya miaka 20
kilivyobatuliwa na Egypt, Iraq na Chile katika kundi lao, tatizo ni
vijana kunyimwa nafasi katika soka la nyumbani”
0 comments:
Post a Comment