Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Klabu ya Monaco imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea, Mnigeria John Obi Mikel ambaye anawindwa na mabingwa wa soka nchini Uturuki Galatasaray pamoja na Trabzonspor.
Monaco ambao walimsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Radamel Falcao aliyekuwa anawaniwa na Chelsea, ikiwa ni mipango yao ya kuiboresha timu yao, sasa wamehamishia mawindo yao kwa Obi ikiwa ni sehemu ya kutafuta viungo bora.
Gala, anayoichezea Tembo, Didier Drogba kwa sasa inahangaika na The Blues kukubaliana na ofa yao ili kumsainisha kiungo huyo kwa dau la uhamisho la pauni milioni 16 ikiwa ni mpango wa kuimarisha nafasi ya kiungo cha kati.
Obi alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2006 baada ya kusajiliwa na kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho, na kwa muda mrefu sasa amekuwa akihusihwa na kujiunga na mabingwa wa England Manchester United na Norwegian side Lyn Oslo.

Lakini Obi ataihama Chelsea baada ya kucheza kwa takribani miaka 6 , wakati huo huo kocha wake aliyemsajili amerejea huku Waturki wakimhitaji kwa nguvu zote.
Endapo nyota huyo raia wa Nigeria ataekekea Uturuki, ataungana na Drogba kwa mara nyingine tena aliyeondoka Chelsea na kujiunga na klabu ya China ya Shanghai Shenhua na sasa yupo Gala ya Uturuki.
Obi amebakisha miaka minne katika mkataba wake wa sasa darajani, lakini ameshaweka wazi kuwa hajui maisha yake ya baadaye na hajui wapi wapi ataelekea. Aliyasema hayo wakati akiwa katika majukumu ya kuitumikia timu yake ya Taifa michuano ya kombe la mabara nchini Brazil

Obi wiki iliyopita alisema: ‘Nimebakisha miaka minne kwenye mkataba wangu na Chelesea, lakini katika soka huwezi kutabiri, siku hii upo hapa, siku inayofuata unaweza kuondoka.’
Wakati huo huo imetuma ofa kwa Sporting Lisbon ili kumsajili nyota wake mwenye umri wa miaka 18, Bruma,

0 comments:
Post a Comment