Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
WAKATI Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich akitimiza miaka kumi ya umiliki wake darajani na kupondwa na baadhi ya makocha kwa sera yake ya kutumia fedha nyingi kununua wachezaji nje ya England na kuwanyima wazawa nafasi ya kucheza, sasa bilionea huyo mwenye kiburi cha pesa amesema anahitaji kuona maendeleo makubwa katika kituo cha kukulea vipaji cha klabu hiyo (Chelesea Academy) ili kuijenga upya timu yake.
Mtandao wa MATUKIO DUNIANI kwa kushirikiana na Sportsmail.com ameinasa kauli ya bilionea huyo kuwa anahitaji kuzalisha wachezaji wa kwake siku zijazo ili kuwarithi wakongwe wa wa klabu hiyo.
Wachezaji wakongwe wakiwemo nahodha John Terry na Frank Lampard – ambao walisainishwa mwaka 2001 kutoka West Ham, mpaka sasa wanaonekana kuwa ni moyo na roho ya klabu, hivyo Abramovicha amedai anatakiwa kuzalisha wachezaji wapya kutoka katika Akademi yake na kuachana na hasara kubwa aipatayo kwa kununua wachezaji wa bei kubwa.
Maboresho yanahitajika: Roman Abramovich anataka wachezaji vijana zaidi kutoka katika Akademi yake ya Chelsea ili kuwarithi wakongwe wanaotamba darajani
Moyo na roho ya klabu: Abramovich, kulia, akishangilia na Frank Lampard, katikati, na John Terry, kushoto, mnamo mwaka 2005
: John Terry, wakati akiwa na miaka 19, ndio mchezaji wa mwisho kinda kusajiliwa na Chelsea akitokea katika mfumo wa soka la vijana na kuwa mchezaji chaguo la kikosi cha kwanza
Kinda la nguvu: Terry enzi za ujana wake katika klabu ya Chelsea career
Lakini kwa sasa, Abramovich anahofia kuwa Chelsea inaweza kuachwa na wakongwe bila ya mchezaji mmoja kutoka katika Akademi yake ambayo amewekeza kiasi cha pauni miliono 100.
Zao ya Akademi: Nyota wa Chelsea Ryan Bertrand, akiwa na meneja wake Jose Mourinho katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpta, nyota huyo ni zao la kituo cha Chelsea 
0 comments:
Post a Comment