Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Miamba ya soka la Tanzania, wekundu wa Msimbazi Simba “Taifa Kubwa” tayari wameshawasili Kahama mkoani Shinyanga wakitokea ziarani Mpanda mkoani Katavi na leo hii asubuhi wanaendela na mazoezi yanayosimamiwa na kocha mtaalamu na mchezaji machachari wa zamani wa klabu hiyo Abdallah Kibaden “King Mputa”.
Akizungumza kwa njia ya Simu na Mtandao wa MATUKIO DUNAINI asubuhi hii kutoka Kahama, kocha msaidizi wa wekundu hao wa Msimbazi, Jamhuri Kiwhelo “Julio Alberto” amesema kwanza wanamshukuru Mungu kwa safari njema kutoka Mpanda mpaka Kahama ambapo leo hii mwalimu ameanza progrmu ya mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kombaini ya Kahama siku ya jumapili.
“Kwanza tunamshukuru mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutupa uzima na kutusafirisha salama, tuko Kahama hapa na ninavyokuambia hizi kocha Kibadeni anapanga program ya mazoezi uwanjani”. Alisema Julio.


“Mpaka sasa wachezaji wote wapo salama licha ya safari ndefu na mizunguko yote, nakwambia hakuna aliyeshikwa hata na homa ndogo, wote wapo salama, na ndio maana tunatanguliza shukurani nyingi kwa mwenyezi Mungu”. Alisema Julio.
Kocha huyo mwenye maneno mengi na kipaji cha ushawishi, alisisitiza kuwa lengo lao ni kuandaa Simba ambayo itawapa raha mashabiki wao msimu ujao ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa.
“Tunasuka kikosi kizuri sana, kwa sasa tuna wachezaji wengi ambao tunawapima kama wana uwezo mzuri ili tuwape mikataba, sisi benchi la ufundi tuko makini kusajili, hatukurupuki kabisa, unaweza kuona kuna wachezaji wengi wa kimataifa na wa hapa nyumbani, usajili bado, tunaangalia nani anatufaa”. Alisema Julio.
Julio alisema baada ya mazoezi ya Kahama na kucheza mechi ya kirafiki jumapili, Simba wataelekea Musoma mkoani Mara ambapo wataweka kambi kwa siku kadhaa na baadaye watasafiri kuelekea nchini Kenya kushiriki michuano ya Ujirani Mwema waliyoalikwa huko.
“Tukitoka Musoma tutaenda Kenya kushiriki mashindano tuliyoalikwa Kenya, lakini tukitoka huko tutarejea tena mkoani Tabora na Katavi kuendelea na kambi, na siku tukirudi Dar es salaam kikosi kitakuwa tayari kwa mapambano ya ligi kuu Tanzania bara, na msimu ujao lazima wapinzania watujue kuwa Simba ni klabu ya kimataifa”. Alitamba Julio.
0 comments:
Post a Comment