Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Wakati mshambuliaji nyota wa majogoo wa jiji ama wekundu wa Anifield, klabu ya Liverpool, raia wa Uruguay, Luis Saurez akiendelea kusisitiza nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo kwa madai ya kutaka kucheza UEFA, beki mpya wa miamba hiyo ya soka, Kolo Toure amemuambia kuwa anaweza kutimiza ndoto zake kwa kuichezea klabu hiyo kwani benchi la ufundi lina mipango mizuri sana ya kuifikisha mbali.
Toure beki wa zamani wa The Gunners, Asernal amesema nia ya Suarez ni nzuri sana, lakini ajua huko anakotaka kwenda mambo yanaweza kuwa magumu afadhali Liverpool, hivyo abaki na kuisaidia timu ili ipate mafanikio makubwa siku zijazo.
Lakini ikumbuke kuwa Toure mnamo mwaka 2009 aliihama Asernal na kujiunga na Manchester City kwa sababu inayofanana na ya Suarez, ila kwa sasa amemshauri nyota huyo raia wa Uruguay kuendelea kuichezea Liverpool ili aonje mafanikio yajayo siku za usoni.


“Kiukweli Luis kama atakubali kubaki, ana nafasi ya kushinda mataji mengi”, alisema Toure. klabu hii inaandaliwa kwa mafanikio, umoja, mpangilio wa mambo kwa viongozi na morali ya wachezaji, ni dalili ya kuijenga upya timu hii, hivyo vyema Luis akabakia.
Toure alisema Liverpool ni timu kubwa sana. Luis ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, ana vitu vingi vya uwanjani. Lakini klabu ndio yenye uwezo wa kufanya maamuzi ambayo yatakuwa mazuri kwa kila mtu.
Nyota huyo raia wa Ivory Coast, ni mchezaji mpya aliyesajiliwa katika majira haya ya joto ya usajili barani Ulaya akitokea Man City alikomaliza mkataba wake, na amepewa nafasi hiyo kuziba pengo la Jamie Carragher aliyetangaza kustaafu soka.


“Ni heshima kubwa kuichezea Liverpool,” alisema Toure. “Nimekaa hapa kwa wiki mbili na kuona mambo mengi mazuri. Nitatoa mchango wote kwa klabu ya Liverpool. Jamie Carragher alikuwa mchezaji muhimu sana na Liverpool wanahitaji mtu wa kuziba pengo lake. Hii ni klabu ya makombe. Nataka kuwa sehemu ya Historia klabuni hapa.”
0 comments:
Post a Comment