Thursday, July 11, 2013


KIKOSI CHA JKT RUVU KILICHOCHEZA NA YANGA .
Na Baraka Mpenja 
Maafande wa Jeshi la kujenga taifa, JKT Ruvu ya mkoani Pwani wamesema baada ya mahangaiko ya msimu uliopita kutafuta kukwepa rungu la kushuka daraja yanatosha na sasa wanayo kazi moja tu ya kujipanga kwa nguvu zotena hakuna kulaza.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI, Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Greyson Haule amesema maandalizi ya msimu mpya yalishaanza mapema, na mpaka sasa wanaendelea vizuri, huku wachezaji wakiahidi kufanya vizuri zaidi msimu mpya na kushika nafasi  nzuri.
“Benchi la ufundi linawaandaa vizuri vijana, morali yao inaridhisha sana, wanaahidi makubwa msimu ujao, hakika tutafanya vizuri sana na kuleta changamoto kubwa zaidi”. Alisema Haule.
Haule alisema kuwa ligi kuu kwa sasa imekuwa ngumu sana kwani timu zote zinacheza soka safi, lakini wao wanatambua hilo na wamejifunza kutokana na makosa yote yaliyowagharimu.
“Safu ya ushambuliaji ilikua butu sana, pia mabeki  walikuwa hovyo sana msimu uliopita, kwa sasa tunasuka safu bora ya kupachika mabao na beki ya kuzuia kufungwa, moto wetu utakuwa mkali sana kwa timu pinzani”. Alisisitiza Haule.
baloziAkizungumzia usajili, Haule alisema bado hawajafanya zozezi hilo kwa muda huu, lakini wanaangalia wapi  wanatakiwa kuongeza wachezaji wengine, na hii inatokana na wachezaji wao wengi kubakia klabuni hapo.
“Kwa mtu yeyote anajiona ni mchezaji wa mpira, tunamkaribisha sana kufanya majaribio JKT Ruvu, akifuzu tutamsajili bila wasiwasi”. Aliongeza Haule.
Haule alisisitiza kuwa nyota wao Musa Hassan Mgunya “Mgosi” ambaye alijiunga nao akitoka DC Motemapembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC na bahati mbaya akakumbwa na majeruhi na hatimaye kurejea uwanjani mechi za mwishoni, atafanya vizuri zaidi msimu mpya na kuwa kiongozi katika safu yao ya ushambuliaji.
“Mgosi bado ni mchezaji mzuri,  ana vitu vingi akiwa uwanjani, majeruhi na kuchelewa kwa kibali cha kucheza ligi kuu msimu uliopita, vilimgharimu sana, lakini kwa sasa anajifua vizuri kabisa na atafanya mazuri”. Alisema Haule.
Wakati Haule akiyasema hayo, naye beki wa kushoto wa klabu hiyo, Stanley Nkomolo alitamba kuonesha kiwango cha juu msimu ujao na kuchukua namba ya mtu timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.
Nkomolo anayejiona kuwa ni beki mzuri wa pembeni kuliko wote aliongeza kuwa kwa maandalizi anayoyafanya binafsi, lazima awe katika kiwango cha juu kwa muda wote.
Beki huyo aliwahi kuzungumza na MATUKIO DUNIANI  siku chache baada ya kumalizika kwa msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara mnamo Mei 18 na kukiri kuwa endapo Simba na Yanga watamhitaji, alikuwa tayari kujiunga nao, lakini kwa bahati mbaya hajapata  ofa yoyote kutoka klabu hizi kubwa nchini Tanzania.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video