Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Washika bunduki wa kaskazini mwa jiji la London, klabu ya Arsenal, wamefufua upya mipango ya kutaka kumsajili na kumrudisha tena London nahodha wao wa zamani na mwanandinga wa wazee wa Katalunya kwa sasa, FC Barcelona, namzungumzia kiungo Cesc Fabregas katika majira haya ya joto.
Nyota huyo wa zamani wa Asernal kwa sasa yupo mapumzikoni akila raha na kuweka akili sawa kufuatia kuwa na msimu mgumu Camp Nou na anapumzika baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Hispania iliyoshindwa kutwaa kombe la mabara baada ya kufungwa na wenyeji Brazil mabao 3-0 katika mchezo wa fainali.
Taarifa za huko Hispnia zinadokeza kuwa nyota huyo bado ana nia ya kubakia Camp Nou, lakini bado wasiwasi umetanda kama ataendana na mipango ya kocha Tito Vilanova, na ikizingatiwa kuwa msimu uliopita alikaa benchi katika baadhi ya mechi kubwa kwa klabu yake.

Kama Wakatalunya watamuuza Fabregas, washika bunduki wa London watakuwa wakwanza kumrejesha nahodha wao kwa usajili wa pauni milioni 25

Wakati huo huo, washika bunduki wa London wameamua kufufua mipango yao ya kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams kufuatia Thomas Vermaelen kurejea katika majeruhi.
Nyota huyo wa Wales anawindwa sana na Arsene Wenger majira haya ya usajili, lakini wameshindwa kufikia dau linalohitajika la pauni milioni 10.
Mtandao wa michezo wa Sportsmail.com ulisema jumanne ya wiki hii kuwa, nahodhaVermaelen atakosa maandalizi ya msimu mpya kutokana na majeruhi, na ataiacha Arsenal ikiwa na mabeki wazima wawili wa kati; Laurent Koscielny na Mertesacker.


Majeruhi ya Thomas Vermaelen yanawalazimu Arsenal kuanzisha mbio za kumsaka Ashley Williams
0 comments:
Post a Comment