Na Baraka Mpenja
Wanandinga
wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mdenish Kim
Paulsen wanatarajiwa kuingia kambini leo katika hoteli ya Tansoma, Dar
es Salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Uganda, The Cranes kuwania tiketi
ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN)
zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza mecihi ya
kukata na mundu dhidi ya wapinzani wao wa karibu, timu ya Taifa ya
Uganda Julai 13 mwaka huu, saa 9:00 Alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Kampala, nchini
Uganda.
Katika
kikosi hicho, kocha Kim Paulsen amemteua kipa Juma Kaseja kuwa kipa
namba moja na nahodha wa timu hiyo licha ya klabu yake ya Simba “Taifa
kubwa” kutangaza kuachana naye.
Kim
akiongea na waandishi wa habari siku ya jana alisema Kaseja bado ana
kiwango cha juu na anafanya kazi yake vizuri akiwa langoni, hivyo ni
lazima awepo katika kikosi chake na kuwa kiongozi.
“Kaseja
ni kipa mzuri, anafanya kazi nzuri kwa timu ya taifa, hivyo nimemuita
katika kikosi changu. Atakuwa kipa namba moja na nahodha. Mimi sijali
kilichotokea klabuni kwake, hayanihusu. Ninachojua bado huduma yake ni
nzuri na ndio maana nimemteua na ataendelea kuwa kiongozi kama kawaida”.
Alisema Kim.
Siku
za karibuni Kim alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa,
ameshangazwa na klabu ya Simba kumtema Kaseja kwani bado ni mlinda
mlango bora kwa sasa nchini Tanzania na hakuna kipa mzuri kama yeye kwa
sasa.
Kim alisema Kaseja ana uwezo mkubwa, pia ni kiongozi mzuri akiwa uwanjani, hivyo ni jambo la ajabu kwa Simba kumuacha kipa huyo.
Wakati
Kim akisema hayo, nao viongozi wa Simba walisema kuwa Kaseja alikuwa na
nyodo sana, mara kadhaa walimuita aende ofisini kuzungumza na viongozi
kuhusu hatima yake ya mkataba ambao ulimazika klabuni hapo, lakini kipa
huyo hakuonesha ushirikiano kwa madai kuwa ana majukumu ya timu ya
taifa.
Baada
ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa, bado Kaseja aliweka ngumu
kutokea mezani, na ndipo viongozi wa Simba wakaamua kuachana naye kwa
madai kuwa labda ana mipango mingine.
Lakini
bado Kocha wa Stars ameponda maamuzi ya kuachwa kwa Kaseja, na kama
sehemu ya kumuamini sana, Jana ametangza kikosi chake na Kaseja ni kipa
namba moja na atakuwa nahodha.
Wachezaji
walioteuliwa na Kocha Mdenmark, Kim Poulsen ni makipa Juma Kaseja
(Simba) , Aishi Manula (Azam), Mwadini Ally (Azam) na Ally Mustafa
(Yanga). Mabeki ni David Luhende (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam),
Shomary Kapombe (simba), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga),
Kelvin Yondan (Yanga), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga),
Haroun Chanongo (Simba), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Mudathiri Yahya
(Azam), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar
(Azam), (Simba),
Washambuliaji ni Simon Msuva (Yanga), Mrisho Ngassa (Simba), John Bocco (Azam).
Kwasasa
Stars inatupian jicho la tatu katika fainali za CHAN baada kutupwa nje
ya michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia nchini Brazil
mwakani baada ya kufungwa na Ivory Coast juni 16 uwanja wa taifa mabao
4-2 na kupoteza matumaini.
0 comments:
Post a Comment