Na Baraka Mpenja
Mabingwa
watetezi wa soka Tanzania bara, wanajangwani Dar Young Aficans,
“Kwalalumpa Malysia” wanaendelea kujifua katika uwanja wa shule ya
sekondari Loyola, Mabibo jijini Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya
msimu mpya wa ligi kuu unaotarajiwa kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka
huu pamoja na michauno ya kimataifa mwakani.
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Baraka Kizuguto amezungumza na mtandao wa MATUKIO DUNIANI na
kusema kuwa kwa sasa ndio wameanza mazoezi chini ya kocha Mholanzi
Ernie Brandts, hivyo kikubwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo
waungane pamoja wakati huu wa maandalizi kwani ndio msingi wa kufanya
vizuri.
“Tumeanza
mazoezi vizuri, tunamshukuru sana mungu mazoezi yanakwenda barabara,
lakini kuna watu wanaandika mambo yao kuwa kuna wachezaji hawapo,
kikubwa watu wawe wanauliza kwanini wachezaji hawapo, sio kuzungumza tu.
Wachezaji wana bosi wao ambaye ni kocha, wajenge utamaduni wa kuuliza
ili wapewe sababu”. Alisema Kizuguto.
Kizuguto
alisema malengo yao ni kujiweka sawa kutetea ubingwa wao pamoja na
kufanya vizuri katika mitanange ya ligi ya mabingwa barani Afirika
tofauti na miaka ya nyuma, na ndio maana wameamua kukazia zaidi mazoezi
ya mapema.
Pia
afisa habari huyo alisema ratiba yao ya kwenda mikoani iko palepale, na
Ijumaa ya kesho kutwa wataanza safari ya kuelekea kanda ya ziwa jijini
Mwnaza ambapo wataonana na mashabiki wao ili kuwaonesha kombe lao
walilotwaa msimu ujao.
“Kikubwa
kwa sasa tunafanya mazoezi, lakini keshokutwa tunaelekea Mwanza kama
tulivyoeleza awali, hakuna kilichoharibika kwa sasa”. Alisema Kizuguto.
Kuhusu
Yanga kususia hafla ya ugawaji wa zawadi inayoendeshwa na wadhamini wa
ligi kuu Tanzania bara, kampuni ya simu ya Vodacom inayotarajiwa
kufanyika leo, Kizuguto alisema maelekezo yao yako palepale na msimamo
ni ule ule.
“Tunahitaji
watufanyie huduma ile ya kutuhamisha pea kabisa, leo hii wanaonesha
mfano wa hundi, tunataka kuona hela yetu imeingia katika akaunti yetu na
baada ya hapo tutashiriki pamoja nao. Lakini kinyume na hivyo sisi
hatutashiriki kwani mfano wa hundi haina maana yoyote kwetu”. Alisema
Kizuguto.
Yanga
walitangaza kususia hafla ya kugawa zawadi za washindi wa ligi kuu soka
Tanzania bara msimu uliopita kwa madai kuwa wadhamini hao wamechelewa
sana ukizingatia ligi ilimalizika tangu mei 18 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment