










……..
Ecobank Tanzania hapo jana jioni iliandaa hafla ya wateja na wafanyabiashara wa Kariakoo katika hoteli ya Valentino. Kitengo cha Fedha Ecobank Tanzania pamoja na tawi la Msimbazi liliwaelimisha wafanyabiashara kuhusu;
- Mbinu za kupunguza garama pamoja na kurahisisha uagizaji kutoka China
- Kufikia masoko yao katika nchi za Afrika mashariki kwa urahisi
- Kupata maoni katika utenda biashara wao na huduma za benki wanazozipata
- Matamanio ya wafanyabiashara na wateja wa Kariakoo
Hii itasaidia pakubwa kurahisisha biashara Kariakoo ambayo ni soko Kubwa Afrika Mashariki na kati. Ecobank pamoja na mtandao wake katika nchi 33 Afrika inawasaidia wateja wao kwa pakubwa kurahisisha kufikia baadhi ya masoko yao, pamoja na hayo Ecobank inasaidia biashara ya uagizaji wa mizigo kati ya Tanzania na China hivo kuwapunguzia garama za uagizaji na ununuzi wa sarafu za kichina RMB moja kwa moja. Hii ni mojawapo ya mbinu katika kampeni ya Ecobank inakuwezesha inayonuia kuinua uchumi wa wananchi binafsi pamoja na biashara kwa kusambaza ujuzi pamoja na kukusanya maoni ya wananchi na biashara ili kutoa huduma zinazoambatana na mahitaji ya jamii.
0 comments:
Post a Comment