Saturday, July 20, 2013


Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Christian Benteke amewashangaza mashabiki wa soka Duniani baada ya kufanya maamuzi magumu ya kufuta maombi yake ya kutaka kuihama klabu yake ya Aston Villa na kuamua kuongeza mkataba mwingine wa miaka minne kuichezea klabu hiyo mpaka mwaka 2017.
Mshambuliajia huyo mwenye umri wa miaka 22, aliomba kuondoka Villa Park wiki mbili zilizopita na ilielezwa kuwa watukutu wa London, Tottenham Huspurs walikuwa wanajiandaa kutuma ofa ya pauno milioni 25  kumsajili, lakini sasa amegeuza dili na kuamua kubakia.
Kocha wa Villa, Paul Lambert , ambaye ni msingi mkubwa wa soka la Benteke kwani alimpa nafasi kwa kutumia nguvu nyingi, aliongea na nyota huyo wakiwa nchini Ujerumani katika ziara ya maandalizi ya ligi kuu soka nchini England na kumtaka kubakia klabuni hapo.
Shake on it: Christian Benteke has revealed he is staying at Aston VillaLete mkono kijana: Christian Benteke amekubali kubakia  Aston Villa
Benteke ameripotiwa kufanya mazoezi jana na amekubali kufuta maombi yake ya kuihama klabu hiyo licha ya Spurs kutangaza kumsajili kwa ada ya pauni milioni 25.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kutoka klabu ya Genk miezi 12 iliyopita, amebakisha miaka mitatu katika mkataba wake ambao anapokea mshahara kidogo wa pauni milioni moja kwa mwaka.
Villa wamekubali kumuongezea mshahara kwa masharti ya kuongeza mkataba. Makubaliano ya leo ni kwamba Benteke atakuwepo Villa Park mpaka 2017 na watamuongezea mara mbili mshahara wake.
Staying put: Benteke was a standout player in his first season for VillaHaondoki: Msimu wa kwanza wa Benteke katika klabu ya Aston Villa ulikuwa mzuri mno
Lambert alisema: “Nilikuwa na mazungumzo mazito na Christian ili arudi mazoezini wiki hii”.
‘Maoni yangu kwake, nilimuambia kitu kizuri ni kuendelea kuichezea Villa”.
“Nimefurahi amechagua kubakia katika klabu yake. Ni zawadi kubwa sana kwangu, pia mashabiki watajisikia furaha kubwa sana kuwa Benteke ataendelea kuichezea klabu yao msimu ujao”.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video