KLABU ya Southampton imekubali kulipa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 kumnunua kiungo Mkenya wa Celtic, Victor Wanyama.
 Watakatifu
 hao, ni miongoni mwa klabu zinazoitaka saini ya Waynama – zikiwemo 
Arsenal, Liverpool na Inter Milan – na sasa wanaingia katika orodha ya 
klabu zinazogombea saini yake. 
 Mpenda kuambaa pembeni: Victor Wanyama anatakiwa na klabu kadhaa kubwa Ulaya
 Yuko juu: Kung’ara kwa kiungo katika Ligi ya Mabingwa kumemfanya amulikwe na wengi
 Kinda
 huyo wa umri wa miaka 21 amekuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa Celtic 
tangu ajiunge na klabu hiyo ya Scotland kutoka Beerschot ya Ubelgiji kwa
 Pauni 900,000 miaka miwili iliyopita.
 Lakini
 Wanyama amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake wa sasa na Celtic 
ambao hawatakuwa na chaguo zaidi ya kukubali faida kumuuza.

0 comments:
Post a Comment