WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
           JESHI LA POLISI TANZANIA
 Anuani
 ya Simu “MKUU 
POLISI”                                                                                                                                       
 
                                                                                                                                                                &
 nbsp;                                      Ofisi ya  Inspekta  Jenerali
 wa Polisi,
Simu
 : (022) 2110734            
                                                                                
             Makao Makuu ya Polisi,
Fax
 Na. (022) 
2135556                                                                     
                                    S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                                   DAR ES SALAAM.
8 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano
 wa  kumi na nane wa mwaka kwa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za
  Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika  Mei 15, 2013   
jijini Dar es Salaam  chini ya mwenyekiti wa umoja huo kwa mwaka 
2012/2013 Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, IGP Said Mwema.
Mkutano
 huo utatanguliwa na Mkutano wa  kamati tendaji za SARPCCO ambao 
 utafunguliwa na IGP Said Mwema  Mei 13, 2013 na kufuatiwa na Mkutano wa
 Wakuu wa Polisi wa nchi hizo utakaofunguliwa Mei 15, 2013 na Waziri wa 
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi.
Katika
 mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana 
na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja na 
ushirikiano baina ya SARPCCO na Umoja wa Wakuu wa Polisi wa nchi za 
Afrika Mashariki (EAPCCO).
Vilevile,
 mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa 
Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na 
kamati tendaji ya Jinsia na watoto katika mkutano wao uliofanyika mwezi 
Machi jijini Dar es Salaam.
Aidha suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo.
SARPCCO
 iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya 
Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya 
uhalifu. Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na nne ambazo 
ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Congo, 
Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland na 
Madagascar.
 Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.





0 comments:
Post a Comment