Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi kupitia vyombo vya habari kutoa taarifa juu ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani itakayofanyika kitaifa Mkoani Rukwa kuanzia tarehe 10 hadi 12 ambapo mgeni rasmi anategemewa kuwa Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi. Soma zaidi juu ya siku hiyo hapo chini baada ya picha.
Timu
 ya wauguzi kutoka Hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ikiwa pamoja na Mkuu 
wa Mkoa wa Rukwa kushoto na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Alhaj 
Salum Mohammed Chima kulia wakati wa kutoa taarifa ya maandalizi ya siku
 hiyo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – Rukwareview.blogspot.com)





0 comments:
Post a Comment