Na Boniface Wambura, TFF
Vyama
 vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa kuendelea na mashindano ya Copa
 Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika 
ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji kutoka 
kwa mdhamini.
 Kwa 
mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola 
ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei 
mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.
 Hivyo,
 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake 
(vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na 
mashindano wakati suala la vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa 
mdhamini wa mashindano.
 Vifaa
 na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika 
kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya 
Tanzania.
 Ni 
matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha
 na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini mashindano 
hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.





0 comments:
Post a Comment