Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Hatimaye ubishi wa timu za Azam Fc wana
lambalamba na wekundu wa msimbazi Simba umemalizika leo hii uwanja wa
taifa baada ya kuchoshana nguvu kwa kufungana sare ya 2-2.
Matokeo hayo, yanaiongezea Azam pointi
moja na kufikisha 47 kibindoni ikibaki nafasi ya pili, nyuma ya Vinara
Yanga wenye pointi 52, wakati Simba wanasalia nafasi ya nne kwa pointi
zake 36, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37 nafasi ya tatu.
Hadi kipindi cha kwanza cha kipute hicho
kulichochezeshwa na mwamuzi Orden Mbaga kinamaliziaka, Mnayama alikuwa
mbele kwa mabao 2-1.
Nyota na Chipukizi wa Simba, Ramadhani
Singano ‘Messi’ alifunga mabao yote mawili kwa upande wa klabu yake
akiunganisha pasi nzuri za winga mwenye kasi Mrisho Khalfani Ngasa
aliyeaambaa na gozi wingi ya kushoto.
Kipre Tchetche aliifungia Azam kwa penalti
dakika ya 29, baada ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kuangushwa kwenye eneo la
hatari na William Lucian ‘Gallas’.
Refa Orden Mbaga alimpandisha jukwaani
kocha Muingereza wa Azam, Stewart Hall dakika ya 31 kwa kutoa maneno
machafu, akilalaimikia uchezeshaji wa refa huyo.
Kipindi cha pili, Azam walirejea kwa nguvu
na kutaka kujinusuru na kipigo na walitimiza ndoto yao baada ya
Humphrey Mieno kuunganisha shuti la mpira wa adhabu lililopigwa na
kiungo Khamis Mcha ‘Vialli`’katika dakika ya 72 na kuzamisha gozi
nyavuni..
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Afisa
habari wa klabu ya Azam Fc Jafar Idd Maganga amesema wamepokea matokeo
kwa mikono miwili kwani ndio soka hilo.
Idd alisema “Tulisema tangu awali kuwa
simba ni wazuri na tulikuwa tayari kupokea matokeo yoyote yale, tumetoa
sare nao lakini tunajipanga kwa mechi zijazo”.
Kwa uapnde wa simba kupitia kwa kocha
msaidizi Jamhuri Kiwhelu Julio alisema bado wanahitaji kupata muda wa
kutosha kwani ndio kwanza timu inaanza kushika kasi.
“Wana Simba tuwe na umoja, timu imecheza
vizuri na tunamshukuru mungu kwa kupata pointi moja na kwa pamoja
tunatakiwa kusonga mbele”. Alisema Julio.
kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel
Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Mussa Mudde, Shomary
Kapombe, Amri Kiemba, Haroun Chanongo/Edward Christopher, Abdallah
Seseme, William Lucian/Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Singano na Mrisho
Ngassa/Fliex Sunzu.
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri
Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Luckson
Kakolaki/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk, Salum Abubakar, John Bocco/Abdi
Kassim, Humphrey Mieno/Jabir Aziz na Kipre Tchetche
0 comments:
Post a Comment