Urejeo wa kiungo bora wa Arsenal Jack Wilshere umewasaidia Arsenal kupata ushindi wa mabao 3-1 ya dakika za lala kwa buriani dhidi ya klabu ngumu ya Norwich City katika dimba la Fly Emirates na kuifanya klabu hiyo ipande nafasi ya nne na kuibua matumaini ya kucheza ligi ya mabingwa ulaya mwakani.
Wikiendi hii Chelsea na
Tottenham hawachezi kwa sababu ya Nusu Fainali ya Kombe la FA, washika
bunduki hao wa jijini London wanaweza kufanya vizuri na kucheza UEFA
msimu ujao hivyo kuondoa machungu kwa mashabiki wake kwani hawana uwez0
wa kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka nchini Englanf msimu huu.
Katika mchezo huo, Norwich
walianza kutikisa nyavu za Arsena kupitia kwa Michael Turner dakika ya
56, lakini kiungo hodari mwenye kiwango kizuri Emirates, Mikel Arteta
akasawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 85, kabla ya
Bassong kujifunga dakika ya 88 na kuipa Arsenal bao la pili, Mjerumani
mwenye sifa ya kufumania nyavu Lukas Podolski alihitimisha kipute hicho
baada ya kuandika bao la tatu na la ushindi dakika ya 90.
Katika mchezo huo, kikosi
cha Arsenal kilikuwa; Fabianski, Sagna/Oxlade-Chamberlain dk80,
Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Arteta, Wilshere/Walcott dk59, Ramsey,
Cazorla, Giroud na Gervinho/Podolski dk59.
Norwich: Bunn, Martin, Whittaker, Bassong, Turner, Johnson/Fox dk62, Snodgrass, Howson, Tettey/Jackson dk90, Holt na Kamara.
Matokeo mengine ya ligi kuu soka nchini England hapo jana ni yalikuwa kama ifuatavyo;
Reading 0-0 Liverpool
Southampton 1-1 Westham united
Everton 2-0 Queens Park Rangers
Aston Villa 0-0 Fullham

Kitu hicho: Mikel Arteta akiisawazishia bao Arsenal kwa penalti

Kipa Mark Bunn akimkoromea mshika kibendera baada ya kuwapa Arsenal penalti


Michael Turner wa akiifungia timu yake bao
0 comments:
Post a Comment