
Mabingwa mara mbili wa kombe la
mapinduzi na makamu bingwa wa kombe la Kagame, klabu ya Azam fc yenye makazi
yake Mbande Chamaz Complex imefanikiwa kufuzu raundi ya tatu ya kombe la
shirikisho licha ya leo hii kutoka suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya
klabu ya Barrack Yc kutoka nchini Liberia.
Akizungumza na matandao huu muda
mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd
Maganga amesema wamepokea vizuri matokeo ya mchezo huo ingawa hesabu zao
zilikuwa kupata ushindi wa nyumbani.
“Mpira wakati Fulani hukataa, leo
bahati haikuwa yetu kabisa, tumejaribu kutengeneza nafasi lakini hatukufanikiwa
kufunga, wengi watajiuliza sana, kila mtu akumbuke kuwa wachezaji walioshindwa
kufunga leo,ndio wale waliofunga mabao mawili kule Monrovia nchini Liberia”.
Alisema Idd.
Idd alisema ushindi wa ugenini wa 2-1
umewafanya wasonge mbele ingawa Barrack Yc walikuwa wanahitaji ushindi kama walivyofanya
kwao, lakini wamekumbana na kisiki cha mpingo leo uwanja wa taifa.
“Baada ya mchezo huo, kocha wetu
mwiingereza Sterwart Jan Hall ameridhika na matokeo, kilichobaki na kuangalia
hesabu za ligi kuu soka Tanzania bara kabla ya kuanza kuwaangalia wapinzani
wetu siku zijazo”. Alisisitiza Idd.
Pia alisema kuwa watanzania wengi
walidhani timu ya Barrack Yc ni nyepesi baasa ya kuwafungwa kwao, lakini
kiukweli ni timu ambayo imejipanga vizuri na ndio maana leo imewatoa jasho
uwanja wa taifa baada ya kutoka nao 0-0.
“Unajua leo kila timu ilakaza kupata
matokeo ya ushindi, tulishambuliana kwa zamu, lakini kwa upande wetu
washambuliaji wetu kama John Bocco, Kipre Herman Tchetche walikosa nafasi za
kufunga, yote kwa yote ni mchezo wa soka bwana”. Alisema Idd.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa
bbaada ya matokeo ya leo, sasa wanajipanga kukutana na timu ya jeshi la
Morroco, kutokea kaskazini mwa bara la Afrika, FAR Rabat ambao ni wagumu
kushindwa.
Katika mchezo huo wa kukata na shoka,
kikosi cha wana lambalamba Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri
Salum, Joackins Atudo, David Mwantika, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum
Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Humphrey Mieno/Abdi Kassim na Brian
Umony/Khamis Mcha ‘Vialli’.
Barack Y.C ya Liberia mashine zao
zilizoanza zilikuwa.; Winston Sayouah, Karleo Anderson, Joseph Broh/Prince
Kennedy, Cammue Tummomie, Prince Jetoh, Junior Barshall, Benjamin Gbamy,
Abraham Andrews, Randy Dukuly/Erastus Wee, Mark Paye na Ezekiel Doe.
0 comments:
Post a Comment