![]() |
Thomas Rosicky |
![]() |
Arsene Wenger kulia |
Jumamosi, 06 Aprili 2013 19:48
>>LEO SARE 1, NYINGINE ZOTE TIMU ZA UGENINI ZASHINDA!!
KATIKA
Mechi za leo za BPL, Barclays Premier League, Arsenal imefanikiwa
kupata ushindi wa ugenini licha ya kucheza Mtu 10 Dakika 20 za mwisho na
kuishusha Chelsea kutoka nafasi ya 4 na wao kuikamata huku Aston Villa
pia walkishinda ugenini na kujikwamua kutoka zile Timu 3 za Mkiani.
PATA TAARIFA KAMILI:
+++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumamosi 6 Aprili
Reading 0 Southampton 2
Norwich 2 Swansea 2
Stoke 1 Aston Villa 3
West Brom 1 Arsenal 2
+++++++++++++++++++++++++
WEST BROM 1 ARSENAL 2
Tomas Rosicky alifunga Bao kila Kipindi
na kuiwezesha Arsenal kuishinda WBA Bao 2-1 ugenini Uwanja wa Hawthorns
katika Mechi ambayo Arsenal walimaliza wakiwa Mtu 10 na kufanikiwa
kuipiku Chelsea nafasi ya 4 katika Msimamo wa Ligi.
+++++++++++++++
MAGOLI:
West Brom 1
-Morrison Dakika ya 71 (Penati)
Arsenal 2
-Rosicky Dakika ya 20 & 50
+++++++++++++++
Mara baada ya Rosicky kuokoa mstarini
jaribio la Claudio Yacob aliifungia Arsenal Bao la kichwa kufuatia krosi
ya Gervinho na Kipindi cha Pili akapiga tena Bao la Pili baada ya shuti
lake kuokolewa na Kipa Foster na Mpira kumrudia tena na kufunga.
James Morrison alifunga Bao la WBA kwa
Penati iliyotolewa na Sentahafu Per Mertesacker ambae alipewa Kadi
Nyekundu kwa kosa hilo la kumwangusha Shane Long.
VIKOSI:
West Brom: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Yacob, Brunt, Dorrans, Morrison, Thomas, Long
Akiba: Myhill, Popov, Rosenberg, Lukaku, Tamas, Fortune, Isaiah Brown.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Rosicky, Ramsey, Gervinho, Cazorla, Arteta, Giroud
Akiba: Mannone, Vermaelen, Podolski, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Jenkinson, Gibbs.
Refa: Howard Webb
NORWICH 2 SWANSEA 2
Bao la 5 Msimu huu la Luke Moore
limewaokoa Swansea City na kupata sare ya 2-2 walipocheza ugenini Uwanja
wa Carrow Road na Norwich City.
Swansea walitangulia kufunga kwa Bao la
Michu lakini Robert Snodgrass akaisawazisha na Kipindi cha Pili Turner
akafunga Bao la Pili kwa Norwich.
+++++++++++++++
MAGOLI:
Norwich 2
-Snodgrass Dakika ya 40
-Turner 60
Swansea 2
-Michu Dakika ya 35
-Moore 75
+++++++++++++++
Matokeo haya yamewaacha Norwich wakiwa nafasi ya 13 na Pointi 4 tu juu ya zile Timu zilizo eneo la kuporomoka Daraja.
VIKOSI:
Norwich: Bunn, Martin, Bassong, Turner, Garrido, Elliott Bennett, Howson, Johnson, Snodgrass, Hoolahan, Kamara
Akiba: Camp, Whittaker, Holt, Fox, Becchio, Ryan Bennett, Tettey.
Swansea: Vorm, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, Ki, de Guzman, Michu, Routledge, Moore, Dyer
Akiba: Tremmel, Hernandez, Lamah, Monk, Shechter, Rangel, Agustien.
Refa: Michael Oliver
STOKE 1 ASTON VILLA 3
Aston Villa wameifunga Stoke City na kujing’oa kutoka zile Timu 3 za mkiani na kuiacha Stoke City ikivutwa kuelekea huko.
Gabriel Agbonlahor ndie aliefunga Bao la kwanza kwa Villa na Michael Kightly kuisawazishi Stoke.
+++++++++++++++
MAGOLI:
Stoke 1
-Kightly Dakika ya 80
Aston Villa 3
-Agbonlahor Dakika ya 9
-Lowton 87
-Benteke 90
+++++++++++++++
Lakini Bao mbili Dakika za mwishoni za Matthew Lowton na Christian Benteke ziliwapa ushindi Aston Villa.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Wilson, Shotton, Nzonzi, Whitehead, Etherington, Walters, Jones
Akiba: Sorensen, Owen, Adam, Kightly, Crouch, Wilkinson, Jerome.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Bennett, Bowery, Delph, Westwood, Weimann, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Given, El Ahmadi, Bent, N'Zogbia, Holman, Sylla, Lichaj.
Refa: Mark Clattenburg
READING 0 SOUTHAMPTON 2
Yale matumaini ya Reading ya kunusurika
kushushwa Daraja yameingia matani baada ya leo kufungwa Bao wakiwa
Nyumbani kwao na Southampton ambao sasa wanaonyesha kuwa wao wamepona
balaa kushushwa Daraja.
Reading, wakiwa chini aliyetimuliwa
Southampton hivi karibuni Nigel Adkins, walianza vyema lakini walififia
baada ya Jay Rodriguez, katika Dakika ya 34, kuifungia Southampton Bao
la kwanza.
Bao la Pili la Southampton lilifungwa na Adam Lallana katika Dakika ya 72.
Hiki ni kipigo cha 7 mfululizo kwa Reading.
VIKOSI:
Reading: Federici, Kelly, Mariappa, Morrison, Gunter, Robson-Kanu, Karacan, Guthrie, Akpan, McAnuff, Le Fondre
Akiba: McCarthy, Pearce, Pogrebnyak, Leigertwood, Hunt, McCleary, Harte.
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Ramirez, Schneiderlin, Cork, Steven Davis, Rodriguez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Fonte, Fox, Ward-Prowse, Lallana, Do Prado, Puncheon.
Refa: Mike Jones
+++++++++++++++++++++++++
RATIBA-BPL:
Jumapili 7 Aprili
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Liverpool v West Ham
[Saa 10 Dak 5 Jioni]
Tottenham v Everton
[Saa 11 Jioni]
Chelsea v Sunderland
Newcastle v Fulham
[Saa 12 Dak 10 Jioni]
QPR v Wigan
Jumatatu 8 Aprili
[Saa 4 Usiku]
Man United v Man City
0 comments:
Post a Comment