Friday, April 19, 2013


lambalamba

Na Baraka Mpenja
Mabingwa mara mbili wa kombe la mapinduzi na wawakililishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa wana lambalamba Azam fc kesho wanashuka dimbani kuwakabili waarabu kutoka nchini Morroco timu ya jeshi ya AS FAR Rabat katika mchezo wa kombe la shirikisho raundi ya tatu.
Mchezo huu wa kukata na shoka utapigwa uwanja wa taifa majira tya saa kumi kamili kwa saa za Afrika mashariki.
Leo hii Makocha wa timu za Azam, Sterwat John Hall na wa FAR Rabat, Abderazzak Khairi watakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mechi hiyo.
Mkutano huo ambao pia utawahusisha manahodha wa timu hizo mbili na utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zilizoko Uwanja wa Karume, Barabara ya Uhuru na Shaurimoyo.
Afisa habari wa klabu ya Azam fc Jafar Idd Maganga aliwata watanzania kuondoa shaka kwani kikosi chao kipo kamili kado kuwavaa maafande hao kutoka milima ya Atlas.
Idd aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi hapo kesho ili kuwashangilia wawakilishi hao wa taifa katika michuano ya kimataifa.
“Tuondoe itikadi za klabu, tujumuike kwa pamoja kupata matokeo ya ushindi, tunawashukuru watanzania watakaojitokeza hapo kesho”. Alisema Idd.
AS FAR Rabat waliwasili jana Dar es Salaam  na kufanya vya hapa na pale.
Kwanza walikuwa ni watu wenye wasiwasi tangu wanatua Uwanja wa Ndege na wasiowaamini wenyeji wao, wakitaka zaidi kujiongoza wenyewe na baadaye sasa wakakataa hoteli waliyokodiwa na wenyeji wao, Sapphire Court.
Pamoja na kuambiwa hoteli hiyo imepitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na timu zote zilizocheza na Azam katika mashindano hayo, zilifikia hapo, Al Nasir ya Sudan Kusini na Barack Young Controllers II ya Liberia, lakini wakagoma.
Wenyeji wakawaambia kama hawataki hoteli hiyo watajilipia popote watakapokwenda na Waarabu hao nao wakaonyesha jeuri ya fedha kwa kujipangia New Africa Hotel. Kaazi kweli kweli.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video