Vyanzo vilivyo karibu na dili hilo
vinasema kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22, aliyeichezea
mechi 22 Ujerumani, atajiunga na timu hiyo mwezi ujao.
Huku mshambuliaji wa Atletico Madrid,
Radamel Falcao pia akitarajiwa kutua Stamford Bridge - licha ya taarifa
za kuhusishwa kuhamia Manchester United wiki iliyopita kwa dau la Pauni
Milioni 45, Chelsea iko tayari kumwaga fedha zaidi kusajili mwishoni mwa
msimu.

Anawindwa: Andre Schurrle wa Bayer Leverkusen

Yupo njiani: Radamel Falcao anaweza kutua Stamford Bridge
Taratibu za uhamisho bado zinaendelea
chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Michael Emenalo, huku klabu pia ikisaka
kiungo mkabaji na kipa namba mbili wa kuchukua nafasi ya Ross Turnbull.
Mzuia michomo wa Ubelgiji, Thibaut
Courtois anapewa uzito wa juu na klabu na ataendelea kucheza kwa mkopo
kwa msimu mwingine Atletico Madrid.
Huku Benitez akiwa tayari amesema
ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu, licha ya mafanikio
aliyoipatia timu katika Kombe la FA na Europa League, kocha wa Everton,
David Moyes, kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho na Manuel
Pellegrini, anayeinoa Malaga kwa sasa, wote wanapewa nafasi ya kutua
darajani.
0 comments:
Post a Comment