 MARA
 baada ya kuchapwa na Manchester United Bao 1-0 hapo jana, Klabu ya 
Sunderland imemtimua Meneja wao Martin O’Neill lakini huko Old Trafford,
 Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, amesisitiza Javier Hernandez 
‘Chicharito’ haendi popote baada ya kuibuka minong’ono kuwa atahama.
MARA
 baada ya kuchapwa na Manchester United Bao 1-0 hapo jana, Klabu ya 
Sunderland imemtimua Meneja wao Martin O’Neill lakini huko Old Trafford,
 Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, amesisitiza Javier Hernandez 
‘Chicharito’ haendi popote baada ya kuibuka minong’ono kuwa atahama.
Sunderland
Klabu ya Sunderland imemtimua Meneja 
wao, Martin O’Neiil, kufuatia kutoshinda katika Mechi zao 8 za Ligi 
zilizopita na kambua Pointi 3 tu kati ya hizo na sasa wako Pointi moja 
tu juu ya zile Timu 3 za mkiani huku Mechi zikiwa zimebaki 7.
++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za chini:
15 Newcastle  Mechi 31 Pointi 33
16 Sunderland  Mechi 31 Pointi 31
17 Wigan  Mechi 30 Tofauti ya Magoli -20 Pointi 30
====================================
18 Aston Villa  Mechi 30 Tofauti ya Magoli -25 Pointi 30
19 QPR  Mechi 30 Tofauti ya Magoli -22 Pointi 23
20 Reading  Mechi 31 Tofauti ya Magoli -25 Pointi 23
++++++++++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, kutimuliwa kwake kumepokewa 
na mstuko na Wadau wengi wa Sunderland ambao wamedai huu si wakati 
muafaka wa kufanya hivyo.
Mmoja wa hao ni Staa wa zamani wa 
Sunderland, Kelvin Kibane, ambae ametamka: “Nimeshangazwa sana. Ni 
uamuzi mbovu katika wakati mbaya! Sidhani kama kuna Meneja anaeweza kuja
 kubadili hapa kabla mwisho wa Msimu!”

FERGIE NA CHICHARITO!
Bosi wa Manchester United Sir Alex 
Ferguson amesisitiza Javier Hernandez ‘Chicharito’ hataondoka Old 
Trafford mwishoni mwa Msimu.
Hadi
 sasa, Chicharito amecheza Mechi 15 za Ligi na kufunga Bao 8 lakini 
amekuwa hapati nama mara kwa mara na Ferguson amekuwa akipendelea 
kuwapanga Wayne Rooney, Robin van Persie na Danny Welbeck.
Jambo
 hilo limezua uvumi kuwa Straika huyo kutoka Mexico huenda akahamia 
Juventus au Real Madrid mwishoni mwa Msimu ingawa pia yapo maneno kuwa 
anaweza kwenda Atletico Madrid ikiwa Straika wao Radamel Falcao atahama 
Atletico.
Hata
 hivyo Ferguson amesema: “Chicharito ana Mkataba wa muda mrefu. 
Hatutazungumza na yeyote kuhusu yeye. Nazungumza na kila Mchezaji hasa 
wale hawachezi kila Siku na nimemwambia ni ngumu kumweka yeye benchi kwa
 vile ana Goli 16.”
Ferguson
 aliongeza: “Yeye kupata namba ni ngumu ukiwa na Wachezaji kama Robin 
van Persie, Welbeck, Rooney na Kagawa. Lakini hii ni bora kwetu ukiwa na
 Kikosi imara, inatupa manufaa sana.”




0 comments:
Post a Comment