
KOCHA MACHACHARI wa Real Madrid Jose Mourinho amedokeza anaweza kurudi kwenye Klabu yake ya zamani bila kutaja jina ni ipi.

Akisisitiza kuwa itakuwa ngumu kwake
kupata Klabu mpya, Mourinho alinena: “Kuna vitu vinaweza kutokea na
hakuna Mtu anaejua. Kila Mtu anajua mie ni mtundu na hii ni ngumu kwa
Familia yangu. Ngoja tuone nini kitatokea.”
Aliongeza: “Ni ngumu kupata sehemu mpya baada ya kuwa Portugal, England, Italy na Spain. Labda ipo sehemu itajirudia!”
Tangu aanze kwenye Ulimwengu wa Soka,
akiwa Mkalimani wa Sir Bobby Robson aliekuwa Kocha Mkuu Barcelona,
Mourinho aliibukia na kuwa Kocha Mkuu wa Klabu za Benfica, Uniao de
Leiria, Porto, Chelsea, Inter Milan na Real.
Mourinho, ambae Mwezi Januari alitimiza Miaka 50, pia alidokeza kuwa ndio kwanza amefikia nusu tu ya maisha yake kama Kocha.
Amesema: “Kama Mungu ataniweka na afya timamu, basi ndio kwanza nipo nusu tu ya maisha yangu ya Soka!”
Pia, Mourinho alisisitiza nia yake ya kuwa Kocha wa Nchi yake Portugal hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment