Na
kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwapo kwenye Uwanja
wa Nou Camp kuona kikosi cha Jose Mourinho kikishinda mchezo huo wa
marudiano baada ya kuanza na sare ya 1-1 nyumbani— kitu ambacho Real
inatumai kukifanya pia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Old
Trafford Jumanne ijayo.
Huo
ulikuwa usiku babu kubwa kwa Mourinho ndani ya Barcelona tangu
aiwezeshe Inter Milan kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa akiwa na
wachezaji 10.

Nyota: Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili Real Madrid ikiifunga Barcelona 3-1 Uwanja wa Nou Camp
TAKWIMU ZA MECHI
Barcelona: Pinto, Alves, Pique, Puyol, Jordi Alba, Sergio, Xavi (Alcantara 74), Cesc (Villa 60), Pedro (Tello 71), Iniesta, Messi.
Benchi: Valdes, Mascherano, Adriano, Song.
Mfungaji: Alba dk89.
Real Madrid: Diego Lopez, Varane, Ramos, Coentrao, Khedira, Cristiano Ronaldo, Ozil (Pepe 79), Xabi Alonso (Essien 84), Arbeloa, Higuain (Callejon 70), Di Maria.
Benchi: Adan,Kaka, Benzema, Modric.
Wafungaji: Ronaldo dk 13 na 57, Varane dk 68.
Mashabiki: 90,002.
Refa: Undiano Mallenco.
Na
ilikuwa mechi ambayo mrithi wa kocha aliyeondoka Barca, Pep
Guardiola,Tito Vilanova alitaka kuanzisha zama mpya za ubabe wao kwa
Real, lakini Ronaldo alizima hilo.
Alimkimbiza
Gerard Pique dakika ya 13 hadi akamchezea rafu kwenye eneo la hatari,
wakati anamlamba chenga na akaenda kupiga mwenyewe hiyo penalti
akimtungua kipa Manuel Pinto na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee
kufunga katika mechi sita za Clasico.
Katika
kipindi cha pili, wakati Barcelona wakitawala mchezo, Angel Di Maria
alimtoka Carles Puyol katika shambulizi lingine la kushitukiza na
alipopiga mira ukarudishwa, ukamkuta Ronaldo, mshambuliaji wa zamani wa
Manchester United tena, akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza
kufunga mabao mawili ugenini katika Clasico.
Katika
mchezo huo, Messi, ambaye aliingia uwanjani kusaka bao la 50 msimu huu,
alifunikwa kama ilivyokuwa kwenye mechi na AC Milan.

Ronaldo akiangushwa chini na Gerard Pique na kuwa penalti akaenda kufunga mwenyewe dakika ya 13

Ronaldo akimpeleka kulia Jose Manuel Pinto, huku mpira ukitinga kushoto


Shujaa: Nyota wa Ureno akishangilia
Messi
alifunikwa na beki kinda Mfaransa, Raphael Varane, na alikuwa bwana
mdogo huyo huyo wa miaka 19 aliyefunga kwa kichwa bao la tatu.
Bao la Varane lilikumbushia bao lake la kusawazisha katika mchezo wa kwanza na lilimsisimua mno Mourinho, ambaye alimvaa beki huyo wa kati kwenye mstari wa kuingia uwanjani na kuanza kushangilia naye.
Bao la Varane lilikumbushia bao lake la kusawazisha katika mchezo wa kwanza na lilimsisimua mno Mourinho, ambaye alimvaa beki huyo wa kati kwenye mstari wa kuingia uwanjani na kuanza kushangilia naye.
Jordi Alba aliifungia bao la kufutia machozi Barca dakika za lala salama akimalizia pasi nzuri ya Andres Iniesta.

Ronaldo akifunga la pili

Mourinho
alimpeleka nje Iker Casillas kukutana na vyombo vya habari mwishoni mwa
mchezo na kuitaka Real Madrid ihakikishe Ronaldo anabaki.
Tetesi
zinamhusisha mchezaji huyo na kurejea England, huku ikisemekana klabu
hiyo haina mpango wa kumuongezea mkataba wake ambao unamalizika mwaka
2015, na Casillas alisema: ‘Ni mchezaji wetu muhimu mno katika mechi
hizi kubwa.
‘Alikuwa tu siyo babu kubwa usiku huu, lakini amekuwa hivyo katika Clasicos nyingine. Ni shujaa wetu.’

Raphael Varane akifungwa kwa kichwa bao la tatu


Varane akishangilia bao lake na kocha Jose Mourinho

Lionel Messi na chini kulia taabani


Jordi Alba akishangilia bao lake la kufutia machozi

Pepe akiwa ameanguka chini baada ya kupambana na wapinzani wake

Sir Alex Ferguson na Msaidizi wake, Mike Phelan walikuwa Nou Camp jana

Mourinho akizungumza na kocha Msaidizi wa Barcelona, Jordi Roura kabla ya mechi
0 comments:
Post a Comment