Tuesday, January 1, 2013

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, leo.

Maalim Seif Sharif Hamad,

Kwa mujibu wa Msemaji wa Kamati ya Mashindano, Farouk Karim, ufunguzi huo unatarajiwa kufanyika usiku na kufuatiwa na mechi kati ya Simba ya Tanzania bara na Jamhuri ya Pemba.
WEKUNDU WA MSIMBAZI KUTOKA TANZANIA BARA
KIKOSI CHA JAMHURI YA PEMBA KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR


Alisema kuwa, mchezo mwingine hii leo utakuwa kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Miembeni, ambao utafanyika kwenye uwanja wa Mao Tsetung kuanzia saa 10 alasiri na kwamba, maandalizi yote yamekamilika, ambapo timu zote shiriki zimeshaanza kuwasili visiwani humo.

Karim alisema kuwa, Januari 4 kutakuwa na mechi mbili, ambapo Jamhuri na Bandari zitacheza saa 10 alasiri na saa 2 usiku, Tusker ya Kenya itakuwa dimbani dhidi ya Simba huku Januari 5, Mtibwa Sugar itapepetana na Coastal Union saa 10 alasiri, wakati Miembeni na Azam shughuli itakuwa saa 2 usiku.

Alisema, mechi nyingine zitakuwa kati ya Tusker na Jamhuri saa 10 alasiri na mechi ya mwisho ya kundi hilo itakuwa kati ya Simba na Bandari wakati kundi B zitakuwa kati ya Miembeni na Coastal Union saa 10 alasiri na mechi ya mwisho katika mzunguko huo wa kwanza ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar.

Karim aliongeza kuwa, hatua ya nusu fainali itaanza Januari 9 kwa mchezo mmoja huku wa pili ukiwa ni Januari 10, ambapo mechi zote zitapigwa saa 2 usiku.

Aliongeza kuwa, fainali za michuano hiyo zitarindima Januari 12 saa 2 usiku, ikiwa ni kilele cha michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
UWANJA WA AMAN MJINI ZANZIBAR

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video