BAADHI ya watumiaji wa simu za
viganjani zenye televisheni ni miongoni mwa watu watakaoathirika na
uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ya mfumo wa analojia.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Mawasialiano nchini (TCRA), akitoa taarifa kuhusu
uzimaji wa mitambo hiyo ya analoji kwenda dijitali, kwa mkoa wa Dar es
Salaam, Injinia Endrew Kisaka alisema hali hiyo inatokana na simu hizo
kuunganishwa na mfumo huo.
Alisema simu hizo zitakosa
huduma hiyo ya matangazo hadi pale kampuni hizo za simu kwa shirikiana
na malaka hiyo kuzindua mfumo utakaokwenda sambamba na dijitali hivi
karibuni.
Injinia Kisaka, alisema uzinduzi
huo unatarajiwa kufanyika haraka ili kuepusha usumbufu unaoweza
kujitokeza kwa watumiaji wa simu hizo.
Akifafanua zaidi kuhusu
changamoto kuhusu ving’amuzi, alisema endapo utatokea usumbufu wananchi
wasisite kurudi sehemu waliko nunua king’muzi hicho kwa maelezo zaidi.
“Unajua kuna baadhi ya maeneo
kama vile yenye majengo marefu na mabonde ambapo maeneo hayo hukosekana
‘signal’ sasa mkiona hivyo rudini kwa wauzaji wenu wawape ushauri wa
kitaalamu utakaosaidia kupata matangazo hayo kwa ubora”alisema Kisaka.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka hiyo, Prof. John Nkoma alisema serikali imejitahidi kuondoa kodi
katika kuingiza ving’amuzi ambapo imesaidia kupunguza bei na kuwa sh
39,000 ambayo anaamini kila Mtanzania atamudu kukipata.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imekuwa ikitoa elimu kwaumma kwa kiwango chakuridhisha,hivyo
uhamaji hautakuwa na usumbufu kwa watumiaji wa huduma za utangazaji.
Pamoja na hayo, alieleza mabadiliko hayo hayatahusu
utangazaji kwa satelaiti, waya (cable) na redio.
0 comments:
Post a Comment