Baada
ya maafande wa Ruvu shooting kushindwa kujipima ubavu na klabu ya Yanga ya Dar
es salaam ijumaa ya wiki iliyopita kutokana na kukosekana kwa uwanja wa
kuchezea mchezo huo kufutaia uwanja huo kutumika na Zambia katika maandalizi ya mechi dhidi ya
taifa stars, maafande hao wamesema wapo tayari endapo Yanga itawahitaji tena
kwa ajili ya mechi hiyo.
KIKOSI CHA RUVU SHOOTING |
Msemaji
wa klabu ya Ruvu shooting Masau Bwire amesema kwa sasa wanaendelea na
maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Bara na kocha mkuu Charles Boniface
Mkwasa Master anaendelea kuwanoa vijana wake ili kupata mafanikio makubwa ngwe
ya lala salama.
Masau
amesema kufuatia vijana wao wawili kuihama klabu hiyo, SEIF ABDALAH aliyeelekea Azam fc na Mlinda mlinda mlango wao namba mbili Musa Gharib kumaliza mkataba
wake wameamua kuchukua vijana wao waliokuwa katika mafunzo ya jeshi.
0 comments:
Post a Comment