Mabingwa
watetezi wa kombe la mapinduzi, klabu ya Azam fc ya Dar es salaam inaendelea na
mazoezi ya kujiandaa kutetea ubingwa wao wa Mapinduzi cup, michuano itakayoanza
kushika kasi januari mosi na kufikia tamati januari 12 mwakani.
![]() |
wachezaji wa Azam Fc |
Afisa
habari wa Azam Jafar Idd Maganga amesema wachezaji wote wapo vizuri na
wanaendelea na mazoezi yao baada ya hivi karibuni kutokea nchini Kongo
walipotwaa ubingwa wa kombe la Hisani la shirikisho la soka nchini humo.
Idd
amesema muda wowote kutoka sasa watatangaza ni lini wanaanza safari ya kuelekea
visiwani Zanzibar tayari kwa kuanza kampeni zao za kutetea ubingwa wao.
Pia
amewataka mashabiki wa Azam kuwa na imani kwani kikosi chao kipo vizuri na
wanajipanga kufanya vizuri kwani itawasaidia kujipanga kwa ajili ya mashindano
ya kimataifa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment