Saturday, June 9, 2018

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa Kassim amewapongeza walimu wa michezo nchini kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutumia muda mwingi kuwaandaa wanafunzi kwa kuwapa utaalam mzuri wa kimichezo ambao kwa sasa wanaonyesha vipaji vyao katika mashindano ya UMISSETA kitaifa.

Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Kassim akizungumza na wadau wa michezo na wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA 2018 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 9 Juni 2018, katika ufunguzi rasmi wa mashindano ya UMISSETA 2018, yenye kauli mbiu “Michezo, Sanaa na Taaluma ni msingi wa maendeleo ya mwanafunzi katika Taifa letu”,ufunguzi uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
“Brass Band” kutoka makutupolo ikiongoza maandamano ya wanafunzi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani kupita mbele ya Mgeni Rasmi kutoa heshima katika ufunguzi wa UMISSETA 2018 jijini Mwanza.
“niwapongeze sana walimu wa michezo nchini kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutumia muda mwingi kuwaandaa wanafunzi kwa kuwapa utaalam mzuri wa kimichezo ambao kwa sasa wanaonyesha utaalam walioupata na vipaji vyao katika mashandano haya ya UMISSETA”,alisema Mh. Majaliwa.
Mh. Majaliwa akikagua timu za mpira wa miguu kama ishara ya ufunguzi wa mashindano ya UMISSETA 2018 yanaoendelea kutimua vumbi katika viwanja vya chuo cha ualimu Butimba na shule ya Sekondari Nsumba jijini Mwanza.
Mheshimiwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipuliza filimbi penati ipigwe kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya UMISSETA 2018 jijini Mwanza.

Aidha mheshimiwa majaliwa ameishukuru kampuni ya chapa ya Coca Cola kwa kudhamini mashindano ya UMISSETA kwa miaka kadhaa sasa, kwani imeweza kuibua vipaji vingi nchini na kulisaidia taifa kuwa na wachezaji mahiri wanaocheza soka la kulipwa ndani na nje ya nchi.
Mh. Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mh. Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya chapa ya Coca Cola.

“niishukuru kampuni ya chapa Coca Cola kwa mchango mkubwa waliouonyesha kwa kudhamini mashindano haya kwa miaka kadhaa sasa, kwani yemekuwa ndio chachu kubwa ya kuibua vipaji vingi nchini na kulisaidia taifa kuwa na wachezaji mahiri wanaocheza soka la kulipwa ndani na nje ya nchi”, alisema Mh. Majaliwa.
Mh. Majaliwa akiteta jambo na Mh. Shonza na katibu wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed S. Kiganja ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maadhimisho ya kitaifa ofisi ya waziri Mkuu.

Ata hivyo mheshimiwa Majaliwa akusita kusisitizia suala la viongozi na wasimamizi wa wanafunzi wakiwemo walimu na maafisa elimu kuwa wanapaswa kuzingatia suala uhalaliwa wanafunzi wanaoshiriki katika mashindano na kuwachezesha wachezaji kutoka nje ya timu walizokuja nazo almaarufu kama mamluki.
Kwa upande wake naibu waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza(mbunge wa viti maalum mkoa wa Songwe),kwa niaba ya mheshimiwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison George Mwakyembe, amemshukuru mheshimiwa waziri mkuu kwa kuona umuhimu wa michezo nchini na kuacha kazi zake na majukumu mengine aliyonayo na kuweza kukubali kuja kufungua mashindano ya UMISSETA 2018.
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo mheshimiwa Juliana Shonza akimshukuru mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuona umuhimu wa michezo na kuweza kufika katika ufunguzi wa UMISSETA 2018 jijini Mwanza.
 


“mheshimiwa waziri mkuu kwa niaba ya mheshimiwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, nikushukuru sana kwa kuona umuhimu wa michezo nchini na kukubali kuacha kazi zako na majukumu mengine uliyonayo ili uweze kuja kufungua mashindano haya ya UMISSETA 2018 hapa jijini Mwanza”,Alisema Mh. Shonza.

Sanaa nayo haikuachwa nyuma Msanii Abdulaziz Chende almaarufu kama Dogo Janja alipata nafasi ya kutumbuiza katika ufunguzi wa UMISSETA 2018 jijini Mwanza.


 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video