Saturday, April 28, 2018

Serikali kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imesema inalojukumu la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini imejipanga kuhakikisha vipaji vya vijana vinaibuliwa kutoka shuleni.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini Mheshimiwa Evod Mmanda akisoma hotuba ya waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Selemani Jafo kwa kadamnasi iliyojitokeza katika uzinduzi wa maandalizi ya UMISSETA 2018 na ugawaji wa vifaa kwa Mkoa wa Mtwara, tukio lililofanyika tarehe 28 April, 2018 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini Evod Mmanda akisoma hotuba ya Mheshimiwa waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo katika uzinduzi wa maandalizi ya UMISSETA 2018 na ugawaji vifaa vya Michezo kwa shule za sekondari, uliofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini Mheshimiwa Evod Mmanda akizungumza na kadamnasi iliyojitokeza katika uzinduzi wa maandalizi ya UMISSETA 2018 na ugawaji wa vifaa kwa Mkoa wa Mtwara, tukio lililofanyika tarehe 28 April, 2018 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

“katika hotuba yake Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI amesema serikali inalojukumu la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini wamejipanga kuhakikisha vipaji vya vijana vinaibuliwa kutoka mashuleni,” Alisema Mmanda.

Aidha katika hatua nyingine Mheshimiwa Mmanda amesema Michezo ni zaidi ya kucheza kwani inatuwezesha kutenda majukumu mbalimbali kwa ushirikiano mwema bila kujali tofauti zozote miongoni mwa wananchi pamoja na kutufundisha ushindani na kutujengea misingi ya kukubali kushinda au kushindwa na kwa matokeo yoyote kuendelea kuwa wamoja.
Timu za shule ya Mikindani na Shule ya SabaSaba zikiingia uwanjani Nangwanda Sijaona katika mechi ya uzinduzi wa maandalizi ya UMISSETA 2018 kwa Mkoa wa Mtwara, ambapo katika mchezo huo Timu ya Sabasaba ilichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja.
“Michezo ni zaidi ya kucheza kwani inatuwezesha kutenda majukumu mbalimbali kwa ushirikiano mwema bila kujali tofauti zozote miongoni mwetu pamoja na kutufundisha ushindani na kutujengea misingi ya kukubali kushinda au kushindwa na kwa matokeo yoyote kuendelea kuwa wamoja,’’ Alisema mheshimiwa Mmanda.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mjini Mh. Evod Mmanda akipiga penati kuhashiria uzinduzi wa maandalizi ya mashindano ya UMISSETA kwa Mkoa wa Mtwara. 


Ata hivyo Mbali na uzinduzi,Mh. Mmanda alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo,Vifaa ambavyo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano hayo,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mjini Mh. Evod Mmanda akigawa vifaa kwa moja ya shule itakayoshiriki katika maandalizi ya mashindano ya UMISSETA mwaka 2018 Jijini Mwanza. 

Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo wa kampuni ya Coca-Cola akisisitiza kuwa wanajivunia kuwa wadhamini wa mashindano hayo kwa kipindi cha miaka 3 mfulilizo na anaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa.

Kwa upande wake Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo,amesema kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuwa mdhamini wa mashindano hayo kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na anaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo wa kampuni ya Coca-Cola akimkabidhi zawadi ya mpira Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Evod Mmanda katika uzinduzi wa ugawaji vifaa vya UMISSETA Mkoani Mtwara.

”Udhamini wetu katika mashindano haya tumejikita katika kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wanaoshiriki kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi ya taifa,kutoa mafunzo kwa makocha wanaofundisha timu na zawadi kwa timu zinazofanikiwa kufanya vizuri”,alisisitiza Sialouise.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video