Saturday, April 7, 2018

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela kuwaagiza watendaji wake kusimamia na kuhakikisha viwanja vilivyogeuzwa kuwa sehemu za kufanyia biashara vinarejeshwa katika hali yake ya zamani ili kuimarisha Michezo na kuupa Mkoa huo nafasi nyingine ya kuandaa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA siku za usoni.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Martin Shigela, kuagiza watendaji wake kusimamia na kuhakikisha viwanja vilivyogeuzwa kuwa sehemu za kufanyia biashara vinarejeshwa katika hali yake ya zamani ili kuimarisha Michezo na kuupa Mkoa huo nafasi nyingine ya kuandaa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA siku za usoni.

Katibu Kiganja ameyasema hayo katika uzinduzi wa maandalizi na ugawaji vifaa vya mashindano ya UMISSETA kwa timu za Mkoa wa Tanga, ikiwa ni mwendelezo wa ugawaji vifaa kwa mikoa mbalimbali itakayoshiriki mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA mwaka 2018 jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela katika uzinduzi wa maandalizi UMISSETA na Ugawaji vifaa uliofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
“Nikuombe sana Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, kuagiza watendaji wako kusimamia na kuhakikisha viwanja vilivyogeuzwa kuwa sehemu za kufanyia biashara na mambo mengine vinarejeshwa katika hali yake ya zamani ili tuimarishe michezo na tuupe Mkoa huu nafasi nyingine ya kuandaa mashindano haya siku za usoni,” Alisema Kiganja.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Martin Shigela, amemshukuru Katibu Mkuu wa BMT kwa kusimamamia vizuri Michezo nchini, sanjari na maombi aliyowasilisha kwake kuhusu kuboresha na kuvifufua viwanja vya Michezo mbalimbali katika mji wa Tanga, na kuhaidi kuyatekeleza maombi hayo ili Mkoa uimarishe Michezo na upate nafasi nyingine tena kuweza kuwa wenyeji wa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela akimshukuru Katibu Mkuu wa BMT kwa kusimamamia vizuri Michezo nchini, sanjari na maombi aliyowasilisha kwake kuhusu kuboresha na kuvifufua viwanja vya Michezo mbalimbali katika mji wa Tanga, na kuhaidi kuyatekeleza maombi hayo ili Mkoa upate nafasi nyingine tena kuweza kuwa wenyeji wa mashindano hayo siku za usoni.

“Nakushukuru sana Katibu Mkuu wa BMT kwa ushauri mzuri uliotupa,kilichobaki sasa ni kuagiza watendaji wangu kuyatekeleza maombi yako kwani tuna shauku kubwa sana na sisi tuweze kuandaa kwa mara nyingine tena mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ambayo mara ya mwisho tuliweza kuandaa mwaka 1999 kama ulivyosema,” Alisema Mhe. Shigela.

Ata hivyo Mbali na uzinduzi,Mh. Shigela alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari zilizokuwepo kwenye uzinduzi huo,Vifaa ambavyo vimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo ni mdhamini mkuu wa mashindano haya,ambapo mwaka huu imepanga kutoa vifaa vya michezo kwa shule 4,000 za sekondari zilizopo sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela (aliyemshika mwanafunzi mkono) akigawa vifaa kwa moja ya shule itakayoshiriki katika maandalizi ya mashindano ya UMISSETA mwaka 2018 Jijini Mwanza.

Mheshimiwa Shigela alisema kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano hayo kutafanikisha jitihada za kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka,mpira wa kikapu na pia kupitia mashindano haya kutaibuliwa vipaji vya wanariadha watakaotamba katika kipindi cha miaka ijayo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Martin Shigela akipiga penati kuhashiria uzinduzi wa maandalizi ya mashindano ya UMISSETA kwa Mkoa wa Tanga

Naye Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo,amesisitiza kuwa kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuwa mdhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka 3 mfulilizo na anaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo wa kampuni ya Coca-Cola akisisitiza kuwa wanajivunia kuwa wadhamini wa mashindano hayo kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo na anaamini vipaji vingi vimeibuliwa na vitaendelea kuibuliwa. 
Meneja wa chapa ya Coca-Cola, Sialouise Shayo wa kampuni ya Coca-Cola akimkabidhi zawadi ya mpira Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela katika uzinduzi wa ugawaji vifaa vya UMISSETA Mkoani Tanga, pembeni kulia ni Meya wa Jiji la Tanga Thobias Mwilapwa.

“Udhamini wetu katika mashindano haya tumejikita katika kutoa vifaa vya michezo kwa wachezaji wanaoshiriki kuanzia ngazi ya mkoa hadi ngazi ya Taifa,”Alisisitiza Sialouise.



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video