Tuesday, February 20, 2018

Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe akielezea kuhusu ujio wa Ujumbe wa FIFA, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Sasan Mlawi akisikiliza kwa makini alichokuwa anakizungumza Mh. Mwakyembe
Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe amesema ujio wa Rais na ujumbe wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA hapa nchini Tarehe 22 Februari 2018, sio ziara ya kuitembelea Tanzania bali ni kikao maalumu ambacho FIFA wameamua kuja nchini kufanya kikao hicho.

Waziri Mwakyembe amesema ujumbe wa FIFA unajumuisha watu 70, tayari baadhi ya ujumbe huo unaanza kuwasili leo tarehe 19 Februari 2018, na Rais wa FIFA atawasili tarehe 21 Februari usiku na kufikia katika hotel ya Kilimanjaro Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini alichokuwa anazungumza mheshimiwa waziri kuhusu ujio wa FIFA
“ni kwamba ujumbe wa FIFA unajumuisha watu 70 na tayari baadhi ya wajumbe wanaanza kuwasili leo Februari 19, 2018 na Rais wa FIFA atawasili tarehe 21 februari usiku na kufikia katika hotel ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam,”Alisema Dkt. Mwakyembe.

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidau akielezea ajenda za Kikao cha FIFA kitakachofanyika nchini Februari 22, 2018

Kwa upande wake katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF Wilfred Kidau, amesema miongoni mwa ajenda kubwa za mwaka huu katika shirikisho la soka Duniani FIFA ni pamoja na kuongelea soka la wanawake Duniani, ya pili ni kuhusu soka la Vijana sanjari na Mradi wa FIFA wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya soka kama vile kujenga hostel za wachezaji vijana katika mataifa mbalimbali duniani n.k.

“Mheshimiwa waziri miongoni wa ajenda kubwa za FIFA katika kikao chao mwaka huu ni pamoja na kuongelea soka la wanawake Duniani, ya pili ni kuhusu soka la vijana Sanjari na Mradi wa FIFA wa kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya soka kama vile kujenga hostel za wachezaji vijana katika mataifa mbalimbali duniani n.k.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video