Tuesday, February 7, 2017

Mechi ya La Liga kati ya Vinara wake Real Madrid na Valencia sasa itachezwa Februari 22 Nyumbani kwa Valencia.
Awali Mechi hii ilikuwa ichezwe Desemba lakini ikifutwa kutokana na ushiriki wa Real huko Japan kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.
Upangwaji upya wa Mechi hii unazidi kuwashushia Real mzigo mkubwa kwani sasa sasa watakuwa na Mechi 8 ndani ya Siku 25 zikiwemo Mechi 2 za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Napoli ya Italia.
Juzi Jumapili, Mechi nyingine ya Real ya La Liga Ugenini na Celta Vigo ilifutwa kutokana na Dhoruba iliyoharibu Paa la Uwanja wa Balaidos na hadi sasa Mechi hiyo haijapangiwa Tarehe mpya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video