Beki wa zamani wa kimataifa wa Uganda Godfrey Kateregga na Saddat Kyambadde wametimuliwa na Police Football Club kwa upangaji matokeo.
“wachezaji hao walikiri,” alisema mwenyekiti wa klabu Assan Kasingye. Wachezaji wengine wamesema namna wawili hao walivyokuwa wakijaribu kuwashawishi mara kwa mara kuuza mechi.
Kasingye amesema, klabu ilifanya kwanza uchunguzi kabla ya kufikia uamuzi.
Kasingye ambaye ni Naibu Inspekta Generali wa Polisi (Assistant Inspector General of Police) na Mkurugenzi wa Polisi wa Kimataifa amesmea: Huu upangaji wa matokeo uliowahusisha wachezaji wazoefu umegundulika ikiwa ni miongoni mwa matatizo ambayo tumekuwa tukikabiliana nayo. Sio tu kwenye klabu yetu, bali pia kwenye vilabu vingine nchini.
Mwezi November, kikosi cha URA FC kinachoshiriki Azam Uganda Premier League kilimsimamisha Kawooya na Oscar Agaba kwa tuhuma za upangaji matokeo.
Mwezi May timu ya SC Villa ambayo ni moja ya timu zenye mafanikio makubwa, ilisimamisha wachezaji wake watano kwa tatizo hilohilo la upangaji matokeo.
0 comments:
Post a Comment