Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, YANGA Sc itamkosa Mlinzi wake wa Kimataifa raia wa Togo Vicent Bossou atakayekuwa nchini Gabon kushiriki michuano ya mataifa barani Afrika (AFCON) kuanzia mwezi January.
Bossou atakuwa akiiwakilsha timu yake ya taifa ya Togo ambayo ipo Kundi C pamoja na timu za Ivory Coast, DR Congo na Morocco.
Mlinzi huyo wa kutegemewa wa Togo anajifua ipasavyo ili kupeperusha vema bendera ya nchi yake.
Bossou amejinasibu kuwa michuano hiyo itamjenga zaidi na kumfanya awe kisiki katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika akiwa na klabu yake ya Yanga, kwani huko ndiko kuna washambuliaji hatari tofauti na hapa kunako Ligi Kuu Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment