Tuesday, November 29, 2016

Jamii ya wapendasoka ulimwenguni kote wameonekana kuguswa na ajali ya ndege iliyohusisha timu ya  Chapecoense ambayo imetokea usiku wa kuamkia leo.

Ndege hiyo iliyoanguka njiani ilikuwa imebeba klabu hiyo ya nchini Brazil kuelekea Colombia kwaajili mchezo wao mkondo wa kwanza wa michuano ya Copa Sudamericana  dhidi Atletico Nacional.

Timu hiyo ilikuwa icheze kunako dimba la Estadio Atanasio Girardot huko Medellin kesho Jumatano lakini ndege yao iliyokuwa ina abiria takriban 72 ilianguka njiani ikiwa Medellin wakati inatoka Santa Cruz de la Sierra huko Bolivia, na kubakisha watu watano tu wakiwa salama.

Mamlaka mbalimbali zimeripoti kuwa maafisa wa ndege hiyo walitangaza hali ya hatari majira ya 22.00 kwa saa za huko baada ya kukumbwa na matatizo ya kiufundi.

Ndege hiyio inasadikiwa kuanguka maeneo ya Cerro Gordo huko manispaa ya La Union

Wanandinga mbalimbali katika ulimwengu wa soka wameamua kutumia akaunti zao za mitandao ya kijamii kutoa pole kutokana na janga hilo la Chapecoense.







0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video