Jana ilikuwa ni siku ya kipekee kwa Cristiano Ronaldo baada ya kusherehekea kufunga magoli 350 akiwa Real Madrid katika mchezo dhidi ya Alaves.
Ronaldo alifunga magoli matatu huku moja likiwa la penati na kukosa penati nyingine na kukamilisha hat-trick yake katika mchezo huo.
Lakini ni magoli mangapi nyota huyo amefunga kwa penati?
Takwimu zinaeleza kuwa asilimia 20 ya magoli yote aliyofunga La Liga amefunga kwa njia ya penati, ikiwa ni idadi ya mabao 53 kati ya 265 ambayo amefunga kwa penati.
Asilimia hizo zimepungua kidogo kwenye Champions League: mabao 10 kati ya 80 sawa na asilimia 25.
Kwenye Copa del Rey (magoli matatu kati ya 21 sawa na asilimia 14.3 amefunga kwa njia ya penati). Hivyo jumla kuwa ni magoli 66 kati ya 371 aliyofunga kwa penati katika kipindi chote alichokuwa Real Madrid.
Maana yake ni kwamba si chini ya 17.8% ya magoli yake, au moja ya tano yanatokana na mikwaju ya penati.
0 comments:
Post a Comment