Sunday, October 30, 2016

Nafikiri mchezo utakuwa na ushinda wa aina yake kwa kuzingatia ubora wa kila kikosi,na nafasi katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mbao FC wanashika nafasi ya 9 kabla ya michezo ya jana wakikusanya alama 13 katika michezo 12 waliyocheza, hivyo wataingia katika mchezo huo wakihitaji alama 3 muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri. Yanga wao wanashika nafasi ya pili wakijikusanyia alama 24 katika michezo 11 waliyocheza ni wazi wataingia katika mchezo huo kusaka alama 3 ili kuendelea kujiweka katika eneo zuri la kutetea ubingwa wao.

Mbao FC wanaotumia mfumo wa 4-4-1-1wakiucheza sana kwenye narrow formation huku wakibadilika kulingana na hali ya mchezo sio timu ya kubeza japokuwa wanaonekana kuwa matatizo ya uchezaji hasa eneo lao la ulinzi.

Safu ya ulinzi ya Mbao FC inaonekana kupoteza umakini na kushindwa kujipanga kwa wakati sio wazuri sana kwenye zonal marking, hivyo katika mchezo wa leo watatakiwa kuongeza umakini na kuchanganya mbinu za ulinzi ili kuweza kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga ambao wanatumia sana penetration passes.

Safu kiungo ya Mbao FC sio wazuri sana kwenye pressing na cut off hivyo uruhusu sana kushambuliwa, kitu ambacho katika mchezo huo watatakiwa kubadilika sana hasa wakizingatia Yanga sio wazuri sana kwenye kiungo hivyo inaweza kuwa faida kwao endapo wakifanikiwa kumiliki katika eneo la kiungo 

Safu ya ushambuliaji ya Mbao FC bado inaonekana sio wazuri sana kwenye kutengeneza nafasi na kuzitumia, kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu kutoka kwa viungo wao ni matatizo yanayoonekana kuikabili safu hii,ni wazi katika mchezo huo watatakiwa kuongeza umakini ili kuweza kuzitumia nafasi chache watazokuwa wametengeneza.

Yanga wanaotumia sana mifumo ya 4-4-2 angle na 4-3-3 vertical wanaonekana kuimarika kiuchezaji baada ya kupita katika hali ya uchovu kwa wachezaji wake. Bila shaka kocha Hans Van de Pluijm ataendelea kujivunia kuzoeleka kwa mifumo na pattens zake za uchezaji.

Safu ya ulinzi ya Yanga inaonekana kucheza kwa utulivu japo hupoteza umakini kidogo na kushindwa kufanya pre-marking hasa wanaposhambuliwa sana. Ni wazi katika mchezo huo watatakiwa kuongeza umakini sana kwa kuzingatia aina ya uchezaji ya Mbao FC.

Safu ya kiungo ya Yanga ni eneo ambalo bado linaonekana kuitesa sana timu hii,kukosekana kwa kiungo wa ulinzi wa maana kumeifanya timu kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu wakati wa kushambulia, sitarajii kuona mabadiliko kwenye safu ni wazi Deus Kaseke, Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima wataendelea kuishikilia timu kwenye idara ya kiungo. 

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inaoneka kurudi kwenye kasi yake iliyozoeleka ni wazi Obrey Chirwa, Simon Msuva na Amiss Tambwe wamekuwa kwenye kiwango bora kwa sasa, hivyo sitarajii kuona mabadiliko makubwa sana kwenye kikosi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video