Kikosi cha Yanga wakubwa leo kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya kikosi cha Yanga B, mchezo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Gymkhana.
Katika mchezo huo ambao ni maalum kwaajili ya kujiweka fiti kuelekea mwendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, magoli ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa kabla ya Donald Ngoma kuongeza la pili na kukamlisha karamu hiyo ya magoli.
Baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Yanga Hans Van der Pluijm amesifu kiwango cha Yanga B na kusema kuwa wamewapa upinzani mkubwa kaka zao.

Picha kwa hisani ya Young African SC
0 comments:
Post a Comment