
Chelsea wamefanikiwa kumrejesha beki wao David Luiz kutoka klabu ya PSG baada ya kuwauzia miaka miwili iliyopita.
Wakati alipokuwa Chelsea mara ya kwanza, Luiz alikuwa akivaa jezi namba 4.
Lakini namba hiyo ilichukuliwa na Cesc Fabregas wakati alipojiunga na Chelsea akitokea Barcelona.
Kufuatia kurejea klabuni hapo katika siku ya mwisho kabisa ya dirisha la usajili, Chelsea wamemkabidhi Luiz jezi namba 30 na Fabregas kubaki na namba yake 4.
Sasa namba hiyo ya jezi imewachanganya sana mashabiki na kujiuliza kwanini beki huyo ameamua kuchagua jezi namba hiyo.
Kupitia kurasa zao za Twitter, hivyo ndivyo mashabiki wa Chelsea waliyokuwa wakijiuliza
0 comments:
Post a Comment