Sunday, September 18, 2016

Pep Guardiola ameieleza Bournemouth kama timu pekee bora ambayo mpaka sasa ameshacheza nayo ikiwa ni wiki moja tu baada ya kukutana na hasimu wake mkubwa Jose Mourinho ambaye anainoa Manchester United.

City walishinda mabao 4-0 dhidi ya vijana hao wa Eddie Howe kwenye Uwanja wa Etihad lakini Guardiola amevutiwa sana kwa namna Bournemouth walivyokuwa wakicheza soka lililokuwa na madhara makubwa kwa upande wake.

Hiki kinaonekana kama kijembe kwa hasimu wake Jose Mourinho, kwani kusema kwamba mpaka sasa timu iliyompa wakati mgumu ni Bournemouth ilhali ameshakutana na United hapo kabla ni kama tusi kwa Mourinho. 

Amesema hivyo huku akianisha kwamba Bournemouth walimletea wakati mgumu kutokana na kucheza soka la chini tofauti na wengine waliokuwa wakicheza mipira ya pasi ndefu.

"Bournemouth ni timu bora miongoni mwa tulizocheza nazo mpaka sasa - walikuwa na madhara makubwa sana pale walipokuwa na mpira, ukilinganisha na timu nyingine zinazocheza pasi ndefu," Guardiola alisema.

"Walitaka wacheze soka safi la chini na ndio maana mfumo wetu wa awali wa kusukuma mashambulizi kwa kasi katika kipindi cha kwanza ulitupa shinda.

"Tuliamua kubadilika na kutumia mipira ya counter-attacks na kutokana na ubora wa viungo na washambuliaji wetu ndipo utofauti ulipotokea."

"Naamini itafikia wakati tutapoteza mechi na kufanya makoa pia, lakini huo ni mchakato."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video