
Jose Mourinho anakabiliwa na mtihani mzito kwenye safu yake ya ulinzi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya mahasimu wao Manchester United wikiendi hii.
Kuna uwezekano mkubwa sana Mourinho akaingia uwanjani siku hiyo bila ya mabeki wake wawili wa pembeni kwenye pambano hilo litakalopigwa Old Trafford, ukiwa ni mchezo wa kwanza dhidi ya hasimu wake mkubwa Pep Guardiola.
Mourinho ana mashaka makubwa juu ya beki wake wa kushoto Luke Shaw , ambaye alilazimika kusitisha mazoezi kwenye kambi ya England kama tahadhari baada ya kupata maumivu ya nyama za mguu.
Kwa upande wa beki wa kulia Antonio Valencia, atachelewa kurudi kutoka kuitumikia timu yake ya taifa Ecuador, ikiwa ni masaa 24 tu kabla ya mchezo huo kufanyika.
Tayari Mourinho atamkosa nyota wake muhimu Henrikh Mkhitaryan, ambaye anauguza majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Romania ilipokuwa ikicheza na Armenia.
Ikiwa hali hiyo itaendelea, basi Mourinho atabidi abadilishe nafasi za walinzi wake kwa kumchezesha Daley Blind kushoto halafu Eric Bailly na Smalling wacheze katikati.
0 comments:
Post a Comment