
Msafara wa Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC unatarajia kuondoka kesho kuelekea Mtwara tayari kuvaana na Ndanda FC Jumatano wiki hii kwenye muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Msafara huo ambao utaondoka saa 11 Alfajiri ya kesho utajumuisha kikosi cha wachezaji 20 na jopo la ufundi chini ya Hans Van Pluijm lenye watu 7.
Katika kikosi hicho wachezaji sita watakosekana kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo matatizo ya kifamilia na kuwa na majukumu katika timu zao za taifa.
Wachezaji wataokao ukosa mchezo huo wa pili wa Young Africans katika ligi ni;
1. Deogratius Munishi ( Msibani )
2. Geofrey Mwashuiya ( majerhi )
3. Pato Ngonyani ( majeruhi )
4. Malimi Busungu ( majeruhi )
5. Haruna Niyonzima ( timu ya taifa )
6. Vicenti Bossou ( timu ya taifa )
0 comments:
Post a Comment