
Meneja wa Arsenal Arsenal Wenger amesema kwamba kukosekana kwa Zlatan Ibrahimovic kwenye klabu ya Paris Saint-Germain ni pigo kubwa kwani wamepoteza mtu ambaye alikuwa zaidi ya mchezaji.
Ibrahimovic amefanikiwa kujitengenezea historia yake PSG baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye klabu hiyo yenye maskani yake Parc des Princes.
Msweden huyo aliondoka PSG mwishoni mwa msimu uliopita na kujiunga na Manchester United.
Wenger amesema: "Wataendelea kuwa timu itakayotawala soka la Ufaransa lakini wamepoteza zaidi ya mchezaji.
"Alikuwa ni kiongozi, nahodha, mwenye kukubali kutokana na mtazamo wake chanya usiopimika klabuni, sasa unapompoteza mchezaji wa aina hiyo ni pigo kubwa.
"Kwa sasa pia wamebadili meneja, hivyo wanajaribu kuendana na mfumo mpya."
0 comments:
Post a Comment